http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Fundi Mbao Atiwa Mbaroni Kwa Kuwabaka Watoto Wake Wawili


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Fundi mbao, Japhet Lendiman (38) mkazi wa Daraja Mbili, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, baada ya kubaka watoto wake wa kike wa darasa la...

wapenzi wa jinsi moja kukosa huduma
Hamad Rashid, wengine sita wateuliwa Uwakilishi
Watumishi hewa 4,317 wafutwa Serikali Kuu

Fundi mbao, Japhet Lendiman (38) mkazi wa Daraja Mbili, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, baada ya kubaka watoto wake wa kike wa darasa la sita na kidato cha kwanza.


Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kiini cha tatizo hilo ni nini na kufuatiwa na hatua ya kufikishwa mahakamani. Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Jeshi la polisi tangu Juni 6, mwaka huu na upelelezi unaendelea kubaini undani wa tukio hilo.


Akimzungumzia mtuhumiwa huyo, mmoja wa majirani wa eneo hilo la Daraja Mbili (jina limehifadhiwa) alidai kuwa mzazi huyo amezoeleka kwa tabia hiyo mbaya mtaani kwao.


Alidai kuwa mtuhumiwa huyo amezoea kubaka watoto wake mara kwa mara wakati mama yao akiwa kazini na kwamba Mei 28 majira ya saa 9:00 alasiri alimbaka tena mtoto wake (Jina tumelihifadhi) wa darasa la sita shule ya Msingi Daraja Mbili ndipo taarifa zilipoanza kuzagaa mtaani.


“Siku hiyo ya tukio lililosababisha mzazi huyo kukamatwa mtoto aliona sasa uvumilivu umefika mwisho, alikwenda kwa mama mkubwa na kutoa taarifa jinsi baba yake anavyomwingilia na kueleza kuwa anataka kunywa sumu ili afe,” alieleza jirani huyo.


Alisema baada ya maelezo hayo mama mkubwa aliamua kuhoji watoto wote wa shemeji yake akiwemo mwingine wa umri wa miaka 14 (jina limeifadhiwa) ambaye yupo kidato cha Kwanza Sekondari ya Felix Mrema, alikiri kuingiliwa na baba yake tangu mwaka 2016.


Aliendelea kueleza kwamba mama yao mkubwa ambaye ni muuguzi (jina limehifadhiwa ) katika moja ya hosptali mkoani Arusha, aliamua kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa na Polisi.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Fundi Mbao Atiwa Mbaroni Kwa Kuwabaka Watoto Wake Wawili
Fundi Mbao Atiwa Mbaroni Kwa Kuwabaka Watoto Wake Wawili
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgOaZrMAXjoV3Mem0DRZ4Ur5gcVDWnZGLQpxFav7g1-gkFgVJRY2Qy6cQOhFK2DJdBk35TLjugs68fwQvZ__Um3I0MBPZFPUhtTZodHfVSt21hhNkVtxweT5qGHUcIAWClmKYTiHIMd5cbB/s1600/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgOaZrMAXjoV3Mem0DRZ4Ur5gcVDWnZGLQpxFav7g1-gkFgVJRY2Qy6cQOhFK2DJdBk35TLjugs68fwQvZ__Um3I0MBPZFPUhtTZodHfVSt21hhNkVtxweT5qGHUcIAWClmKYTiHIMd5cbB/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/06/fundi-mbao-atiwa-mbaroni-kwa-kuwabaka.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/06/fundi-mbao-atiwa-mbaroni-kwa-kuwabaka.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy