http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

WAKURUGENZI WATEULE WAWASILI DODOMA KULA KIAPO


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Mmoja wa wakurugenzi wateule Bw.Hudson Stanley Kamoga Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu. ……………………………………………………………………………….. Na Eleuteri Mangi, MA...

Anna Mgwhira avuliwa uenyekiti ACT- Wazalendo
Yule Mwanamuziki aliyeimba "Kila munu ave na kwavo" afariki Dunia
Halima Mdee: Porojo za Dodoma haziniumizi Kichwa




Mmoja wa wakurugenzi wateule Bw.Hudson Stanley Kamoga Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.

………………………………………………………………………………..

Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma.

Wakurugenzi wa Halmashauri ya Mji, Manispaa na Wilaya, walioteuliwa siku ya Jumamosi Septemba 10, 2016 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wametakiwa kuwasilisha nakala halisi za vyeti vyao vya taaluma, kabla ya kuapa.

Zoezi la uhakiki wa vyeti hivyo litakalofanyika Ofis ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika jengo la Mkapa mjini Dodoma siku ya Jumanne Septemba 13, 2016 kabla ya kuanza kwa zoezi la kuapa.

Wakurugenzi hao 13 ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa mmoja, Mkurugenzi wa Mji mmoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, wanatakiwa kuwasili Ofisi ya Rais TAMISEMI mjini Dodoma saa 2:00 asubuhi kwa ajili ya uhakiki wa vyeti vyao vya taaluma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe na kusainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Rebecca Kwandu, Septemba 11, 2016 inawataka Wakurugenzi hao kuhakikisha wanawasilisha nakala halisi ya vyeti vyao vya taaluma kwa ajili ya kiapo cha uadilifu wa uongozi wa umma.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa uhakiki wa vyeti halisi vya kitaaluma, unafanywa kwa lengo la kujiridhisha baada ya mchakato wa kawaida wa uhakiki kufanywa kwa kutumia vyeti visivyokuwa halisi yaani vivuli.

Wakurugenzi hao ni Godwin Emmanuel Kunambi Manispaa ya Dodoma, Elias R. Ntiruhungwa Mji waTarime, Mwantumu Dau Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Frank Bahati Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Hudson Stanley Kamoga Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Mwailwa Smith Pangani, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Godfrey Sanga, Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama na Yusuf Daudi Semuguruka Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga.

Wakurugenzi wengine ni Bakari Kasinyo Mohamed Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Juma Ally Mnweke Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Butamo Nuru Ndalahwa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Waziri Mourice Halmashauri ya Wilaya ya Karatu na Fatma Omar Latu Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : WAKURUGENZI WATEULE WAWASILI DODOMA KULA KIAPO
WAKURUGENZI WATEULE WAWASILI DODOMA KULA KIAPO
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2016/09/kamoga-1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/wakurugenzi-wateule-wawasili-dodoma.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/wakurugenzi-wateule-wawasili-dodoma.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy