Halila Tongolanga, mwanamuziki mkongwe ambaye alikuwa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam toka wiki il...
Halila Tongolanga, mwanamuziki mkongwe ambaye alikuwa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam toka wiki iliyopita, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Tongolanga, aliyejipatia umaarufu kwa wimbo wa "Kila munu ave na kwavo" alikuwa amesafirishwa kutokea Ndanda kuja Muhimbili akihisiwa kuwa na matatizo ya figo.
Jana Jumapili ililazimika kuanza kufanya jitihada za kupata daktari ambaye angemshughulikia kwa karibu zaidi, na daktari alipatikana ambaye aliahidi angeanza kufwatilia swala lake leo asubuhi lakini mapenzi ya Mungu yalikuwa tofauti.
Juzi alinukuliwa akisema kuwa ana mengi ya kutaka kusema, lakini moja aliloweza kutamka ni kuwa yeye anajihisi ana kansa. alipoulizwa anajuaje hilo, kwa vile hajapimwa hakuwa na jibu
Wengi tutamkumbuka Tongolanga kwa wimbo wake wa Kimakonde aliouimba kwa mara ya kwanza akiwa na Les Mwenge 'Kila Munu Ave Na Kwavo", na baadaye akafanya remix na Makondeko band.
Mwili wa marehemu unategemewa kusafirishwa leo saa tano kuelekea kwao Newala kwa mazishi. Habari zaidi zitawafikia kupia hapa
Mungu amlaze Pema peponi Halila Tongolanga



