http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Trump sasa anaamini Obama alizaliwa Marekani

Image copyri Image capti Bw Trump amekuwa  Afisi ya kampeni ya mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump imetoa ...

Image copyri
Image captiBw Trump amekuwa 
Bw Trump amekuwa akisema haamini Rais Obama alizaliwa Hawaii
Afisi ya kampeni ya mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump imetoa taarifa ikisema sasa anaamini Rais Obama alizaliwa nchini Marekani.
Hilo limetokea saa chache baada ya mahojiano na Bw Trump, ambapo mgombea huyo kwa mara nyingine alisisitiza kwamba hayuko tayari kuamini kwamba Bw Obama alizaliwa Marekani. Akihojiwa na gazeti la Washington Post, Bw Trumo alikataa kusema Bw Obama alizaliwa Marekani na badala yake akasema hangejibu swali hilo.
Bw Trump huchukuliwa mwanzilishi wa kundi lijulikanalo kama "birther movement", ambalo huamini Rais Barack Obama hakuzaliwa katika jimbo la Hawaii, na kwa hivyo hakufaa kuhudumu kama rais wa Marekani.
Mwandishi wa BBC Anthony Zurcher anasema hatua hiyo itakuwa kubwa na sasa huenda ikasitisha mzozo huo.
Anasema taarifa hiyo iliyotiwa saini na mshauri mkuu wa Trump Jason Miller hata hivyo si kwamba anakubali makosa.
Badala yake, anasema, Bw Miller aliweka lawama kwa Hillary Clinton na kundi lake la kampeni la mwaka 2008, ambapo Bi Clinton alikuwa anashindania tiketi ya chama cha Democratic na Bw Obama.
Hakuna ushahidi wa kumhusisha Bi Clinton na kundi la Birther.
Akijibu, Bi Clinton alisema kupitia Twitter kwamba mrithi wa Rais Obama "hawezi kuwa mtu aliyeongoza kundi la ubaguzi wa rangi la Birther".
Wanaopinga kwamba Bw Obama alizaliwa Marekani wamekuwa wakisema alizaliwa Kenya (babake Bw Obama alikuwa Mkenya).
Taarifa katika magazeti kadha ya Marekani zinaashiria uvumi huo ulienezwa mwaka 2008 na wafuasi sugu wa Bi Clinton ilipoanza kudhihirika kwamba mwanamke huyo hangeshinda uteuzi wa chama cha Democratic.
Madai hayo baadaye yalifufuliwa na wafuasi wa mgombea wa Republican John McCain alipoanza kuachwa nyuma na Bw Obama kwenye kura za maoni, tovuti ya Fact Check imeripoti.
Bw Obama
Image copyr
Bw Trump alianza kujihusisha na suala hilo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2012.
Aprili 2011, alimtaka Bw Obama kuonyesha hadharani cheti chake cha kuzaliwa, wito ambao uliungwa mkono na wanasiasa wengi wa Republican akiwemo aliyekuwa gavana wa Alaska Sarah Palin.
Mwaka 2012 mgombea wa wakati huo wa Republican Mitt Romney alirejelea madai hayo kwenye mkutano wa kampeni Agosti mwaka huo.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Trump sasa anaamini Obama alizaliwa Marekani
Trump sasa anaamini Obama alizaliwa Marekani
http://ichef.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/0A1F/production/_91219520_9d498839-f3f6-4456-99ef-81b62dc5a63b.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/trump-sasa-anaamini-obama-alizaliwa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/trump-sasa-anaamini-obama-alizaliwa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy