http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Tanzania yaongoza duniani kwa utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia simu


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza duniani kufanikiwa katika utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia mitandao ya simu. Hayo yameelezwa ja...

CUF Yataka Waziri mkuu Kassim Majaliwa Aombe Radhi
BREAKING NEWS: Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Waziri Wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga Baada Ya Kuingia Bungeni Akiwa Amelewa
Gardner Amjibu Lady Jay Dee, Agoma kuomba Radhi




Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza duniani kufanikiwa katika utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia mitandao ya simu.


Hayo yameelezwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Eng. James Kilaba katika mkutano wa kimataifa wa wadau wa mawasiliano ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (ITU) kwa kushirikiana na TCRA pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BOT).


“Huduma za kifedha kwa mfumo wa digitali nchini Tanzania imepiga hatua kubwa ,ni nchi ya kwanza tuseme ulimwenguni kwa kutuma fedha na kutoa kwa njia ya simu bila matatizo yoyote, pia kuna mfumo wa kutuma fedha benki kwa kutumia mitandao ya simu,” alisema.


Kuhusu mkutano huo wa kimataifa ulioshirikisha washiriki zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali duniani ambazo ni wanachama wa ITU, alisema umelenga kujadili namna ya kufikisha huduma za kifedha kwa njia ya simu katika sehemu ambazo hazifikiwi na huduma hiyo.


“Mkutano huu unasimamiwa na shirika la mawasiliano duniani ITC ambao umelenga kujadili namna ya kutumia mitandao ya simu kupeleka huduma za kifedha katika maeneo yasiyofikiwa na huduma za kifedha hasa ambako hakuna mabenki. Mkutano huu nchi imeamua kuuanda kwa ushirikiano wa TCRA na BOT, ” alisema.


Naye Gavana Mkuu wa BOT Profesa Benno Ndulu alisema hadi mwisho wa mwezi Julai mwaka huu takribani watanzania milioni 21.5 nchi nzima wanatumia huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu.


“Hadi kufikia Julai, 2016 watanzania 21.5 milioni wanatumia mitandao ya simu walau mara 1 kwa mwezi idadi hii ni kubwa na kwamba inaonesha sekta hii inakua kwa kasi,” alisema.


Profesa Ndulu alisema kuwa huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu imesaidia kukuza uchumi wa nchi.


“Malipo ya fedha kwa njia ya simu yanasaidia kupunguza gharama hivyo na kuwa kichochea cha maendeleo, sasa hivi wafanyakazi, wakulima, wanaotumia huduma za bima, wanaonunua bidhaa hulipa kwa Kutumia simu za mkononi hususani kwamba muda ndio muhimu,”alisema.


Aliongeza kuwa “Mitandao ya simu haiathiri huduma za kibenki, na benki wamechangamkia kutumia mitandao kufikia wateja wao, hutumia mawakala kufungulia account, mitandao hii husaidia benki kufikia wateja kote nchini, woga huo umepungua kwa sasa,”

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Tanzania yaongoza duniani kwa utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia simu
Tanzania yaongoza duniani kwa utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia simu
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjwIYkSDcExN6GgM1w2w3a9b8vjjTzZRviJ-I7-HZClM1-w2Z3hM7204PJFpvWgPc-QG5nh5fSi065IFfd2VNd9hvdEHTbSGXVY4N3SfHTmj8ycjXIXzsehxhtkisIPamAitFY3aIAfWRY/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjwIYkSDcExN6GgM1w2w3a9b8vjjTzZRviJ-I7-HZClM1-w2Z3hM7204PJFpvWgPc-QG5nh5fSi065IFfd2VNd9hvdEHTbSGXVY4N3SfHTmj8ycjXIXzsehxhtkisIPamAitFY3aIAfWRY/s72-c/1.JPG
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/tanzania-yaongoza-duniani-kwa-utoaji-wa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/tanzania-yaongoza-duniani-kwa-utoaji-wa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy