http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

ACT-Wazalendo waitisha mkutano wa kidemokrasia Kupigania Upatikanaji wa Katiba Mpya

Chama cha ACT- Wazalendo kimepanga kuwasha moto mjadala wa Katiba mpya katika mkutano wake kidemokrasia kilioitisha jijini Dar es Salaam...



Chama cha ACT- Wazalendo kimepanga kuwasha moto mjadala wa Katiba mpya katika mkutano wake kidemokrasia kilioitisha jijini Dar es Salaam Oktoba 8.


Mkutano huo unalenga kufufua mchakato wa Katiba Mpya kwa kuzingatia michakato ya katiba za nchi nyingine za Afrika, alisema Katibu wa itikadi na uenezi wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu alipozungumza na waandishi jijini Dar es Salaam jana.


Alisema katika kupata uzoefu, ACT Wazalendo imemualika Adabu Namwamba, ambaye ni kiongozi wa Chama cha Labour cha Kenya kilichofanikiwa kubadilisha katiba yake baada ya mchakato mrefu.


Aliwataja wageni wengine kuwa ni mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba ambaye naye atatoa mada kuhusu suala hilo.


Mchakato wa kuandika Katiba mpya nchini umekwama katika hatua ya kupiga Kura ya Maoni baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kushindwa kukamilisha uandikishaji wapigakura kwa muda uliotakiwa.


Mchakato huo uligubikwa na vikwazo kadhaa, ikiwa ni pamoja na vyama vinne vya upinzani na baadhi ya wajumbe kususia kwa maelezo kuwa Bunge liliacha Rasimu ya Katiba iliyokuwa na maoni ya wananchi na kuingiza sera za CCM.


Katika mkutano huo, kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe atawasilisha mada kuhusu hali ya nchi kwa mtazamo wa chama hicho.


“Kiongozi wetu atawasilisha uchambuzi mpana wa kina zaidi kuhusu hali ya nchi yetu kiuchumi, kisiasa na kijamii tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani,” alisema.


Pia, mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Anna Mghwira, ambaye aligombea urais mwaka jana, ataeleza uzoefu wake katika uchaguzi, wakati mshauri wa chama hicho, Profesa Kitila Mkumbo atachambua mwelekeo wa chama hadi mwaka 2020.

“Chama kinatoa wito kwa wananchi wanaotaka kushiriki katika mkutano huo kuwasiliana na ofisi ili kujiandikisha,” alisema.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : ACT-Wazalendo waitisha mkutano wa kidemokrasia Kupigania Upatikanaji wa Katiba Mpya
ACT-Wazalendo waitisha mkutano wa kidemokrasia Kupigania Upatikanaji wa Katiba Mpya
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjGQed18_ZR7RMDCW4LUjTXUfblMdP-AF7FZyWP4FYZvIJCNdx31PCl8gR0v0InrDaJJW5VXJqymaBWI-Hq4tUa0VwMQvV11Tkc4Sc_LEFtV4KtVl0IQx2D7YbPaQRf3HlSeHZ5BDss5bE/s640/2.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjGQed18_ZR7RMDCW4LUjTXUfblMdP-AF7FZyWP4FYZvIJCNdx31PCl8gR0v0InrDaJJW5VXJqymaBWI-Hq4tUa0VwMQvV11Tkc4Sc_LEFtV4KtVl0IQx2D7YbPaQRf3HlSeHZ5BDss5bE/s72-c/2.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/10/act-wazalendo-waitisha-mkutano-wa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/10/act-wazalendo-waitisha-mkutano-wa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy