http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Mwizi Wa Pikipiki Afariki Dunia Baada ya Kupigwa Nyundo Kichwani Wakati Akijaribu Kupora Pikpiki


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Chiza Dastan (31), anayesadikiwa kuwa mwizi wa pikipiki amefariki dunia Hospitali Wilaya ya Bukombe akipewa matibabu baada ya kupigwa ...

Mikataba 9 Tanzania na Uturuki yasainiwa
Zitto Asakwa na Polisi kwa Uchochezi, Dereva Wake na Katibu wa Chama Wakamatwa
Njemba aua wawili na Sita kujeruhi

Chiza Dastan (31), anayesadikiwa kuwa mwizi wa pikipiki amefariki dunia Hospitali Wilaya ya Bukombe akipewa matibabu baada ya kupigwa na nyundo kichwani wakati akijaribu kupora pikipiki.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema tukio hilo lilitokea Mei 20 saa 4.00 usiku nje ya Baa ya Geen View, Kata ya Katente wilayani Bukombe.

Mwabulambo alisema Chiza ambaye ni mkazi wa Kilimahewa, alifariki dunia wakati akitibiwa baada ya kujaribu kupora pikipiki ya Nassoro Tadeo aliyemkodi kutoka mjini Ushirombo kwenda kwenye baa hiyo.
 Alisema wakiwa nje ya baa, ghafla mhalifu alianza kuongea na watu wasiojulikana kwenye simu, mwendesha bodaboda alishtuka na kutaka kuondoka.

Mwabulambo alisema wakati akijaribu kuondoka, Chiza alichomoa nyundo na kuanza kumshambulia mwendesha bodaboda na kumjeruhi kichwani.

Baada ya mwendesha bodaboda kupigwa nyundo kichwani, aliachia pikipiki na kuanza kupambana naye akig’ang’ania nyundo huku akiomba msaada.

Chiza alipanda pikipiki ili aondoke lakini mwendesha bodaboda, alifanikiwa kumnyang’anya nyundo na kuanza kumshambulia.

“Chiza alipoona kipigo kimezidi aliiachia pikipiki na kukimbia kusikojulikana, mwendesha pikipiki alichukua mali yake kwenda polisi ili kuandikiwa PF3 kwa ajili ya kwenda Hospitali ya Wilaya ya Bukombe kupatiwa matibabu,” alisema.

Mwabulambo alisema mwendesha bodaboda kupewa PF na kwenda kutibiwa, akiwa hospitalini hapo alishtuka kuona Chiza akifikishwa na wasamaria wema saa 8.00 usiku akiwa na jeraha kubwa kichwani.

“Lakini kabla polisi hawajatoa PF3 walimhoji na kubaini kuwa, ndiye aliyejaribu kuiba pikipiki,” alisema Mwabulambo.

Hata hivyo, Mwabulambo ametoa wito kwa waendesha bodaboda kuwa makini wanapokuwa kwenye shughuli zao, hasa nyakati za usiku na kwamba wanapomhisi mtu watoe taarifa kituo chochote cha polisi.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk Mahona Kaji alisema majeruhi alipokelewa akiwa na hali mbaya kutokana na kupondwa na kitu kizito kichwani, fuvu la kichwa lilionekana limepasuka. Dk Kaji alisema walijitahidi kuokoa maisha yake lakini ikashindikana.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mwizi Wa Pikipiki Afariki Dunia Baada ya Kupigwa Nyundo Kichwani Wakati Akijaribu Kupora Pikpiki
Mwizi Wa Pikipiki Afariki Dunia Baada ya Kupigwa Nyundo Kichwani Wakati Akijaribu Kupora Pikpiki
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEipQ1fxtKMbyXmD0-p2ePoQxZOtApxmVtfTu-TDWcZrATUh4mAgJObs3IbnouFtU41dItcghUpP9_lBgiXz585svRYfOtx9SF1hr56uYcPTojtOt6zZD0bpboFQyMzBPTajLTWswyW8lS09/s1600/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEipQ1fxtKMbyXmD0-p2ePoQxZOtApxmVtfTu-TDWcZrATUh4mAgJObs3IbnouFtU41dItcghUpP9_lBgiXz585svRYfOtx9SF1hr56uYcPTojtOt6zZD0bpboFQyMzBPTajLTWswyW8lS09/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/05/mwizi-wa-pikipiki-afariki-dunia-baada.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/05/mwizi-wa-pikipiki-afariki-dunia-baada.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy