http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Mikataba 9 Tanzania na Uturuki yasainiwa

Bendera za Uturuki na Tanzania Nchi za Tanzania na Uturuki leo zimetiliana saini mikataba tisa ya ushirikiano katika nyanja mbalimb...


Bendera za Uturuki na Tanzania




Nchi za Tanzania na Uturuki leo zimetiliana saini mikataba tisa ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo leo baada ya kuwasili kwa Rais wa Uturuki kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.


Akizungumza baada ya kutiliana saini mikataba hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amesema, ujio wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan umejumuisha wafanyabiashara 150 na kwamba, mikataba iliyosainiwa itasaidia kukuza uchumi pamoja na mahusiano baina ya mataifa hayo mawili.

Rais Magufuli ameitaja baadhi ya mikataba iliyosainiwa kuwa ni ya sekta za afya, elimu, ulinzi, na viwanda ambapo amesema, amemuomba Rais Erdogan kuikopesha Tanzania kiasi cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge yenye urefu wa zaidi ya kilometa 400.

Rais Magufuli pia amesema Rais huyo wa Uturuki amekubali kuongeza nafasi za wanafunzi wanaokwenda kusoma nchini Uturuki kutoka idadi ya wanafunzi 48 iliyopo hivi sasa, na katika masuala ya ulinzi, amesema Uturuki imekubali kutoa mafunzo ya ulinzi kwa watanzania nchini Uturuki.

Hadi sasa kampuni 30 za Uturuki zimefanya uwekezaji nchini Tanzania wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 305.08 na zinatarajiwa kutengeneza ajira 2,959 na hadi kufikia Februari 2016 biashara kati ya nchi hizi mbili iliongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 66 sawa na shilingi bilioni 145.2 mwaka 2009 na kuwa Dola za Kimarekani milioni 160 sawa na shilingi bilioni 352.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mikataba 9 Tanzania na Uturuki yasainiwa
Mikataba 9 Tanzania na Uturuki yasainiwa
http://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2017/01/23/uturuki%20na%20Tanzania%20bendera.jpg?itok=n7RGxoxl×tamp=1485176601
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/01/mikataba-9-tanzania-na-uturuki-yasainiwa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/01/mikataba-9-tanzania-na-uturuki-yasainiwa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy