http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Mtoto wa Chacha Wangwe Abadili Msimamo Mahakamani


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa machachari na Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, amebadili msimamo mahakamani katika kesi ya kuchapish...

Joshua Nassari: Nipo tayari kujiuzulu Ubunge
VIDEO:TAARIFA Lema kumchongea Nassary afukuzwe ubunge
TUNDU LISSU KUFANYIWA UPASUAJI MWINGINE LEO....


Mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa machachari na Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, amebadili msimamo mahakamani katika kesi ya kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii, kuwa Zanzibar inakandamizwa na Tanzania Bara na kwamba ni koloni lake.



Mtoto huyo, Bob Chacha Wangwe (24), ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alibadili msimamo jana aliposomewa shtaka hilo kwa mara ya pili, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.



Wangwe alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Mei 11, na alisomewa shtaka linalomkabili na alikiri kutenda kosa hilo.



Mshtakiwa anapokiri kosa, kwa kawaida Mahakama inaweza kumtia hatiani na kumpa adhabu kwa mujibu wa sheria, kulingana na kosa siku hiyo hiyo au siku nyingine yoyote.



Baada ya kusomewa shtaka na kukiri, Hakimu Mkazi Mkuu, Waria lwande Lema, aliamuru mshtakiwa huyo apelekwe rumande hadi jana, Mei 17, kwa kuwa hakimu aliyepangwa kusikiliza kesi hiyo hakuwapo.



Hata hivyo, jana mshtakiwa huyo alipopandishwa kizimbani na kusomewa shtaka hilo, ili kusomewa maelezo ya awali kabla ya Mahakama kumtia hatiani na kumhukumu, tofauti na siku ya kwanza, alikana kutenda kosa hilo.



Kutoka na mshtakiwa huyo kukana kosa, Wakili wa Serikali, Salim Msemo, aliieleza Mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika, hivyo aliiomba ipange tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo.



Wakili wa mshtakiwa huyo Peter Kibatala aliiomba Mahakama impe dhamana kwa kuwa shtaka linalomkabili linadhaminika, maombi ambayo yalikubaliwa na aliachiwa kwa dhamana na kesi iliahirishwa hadi Juni 15.


Wangwe ambaye baba yake kwa sasa ni marehemu, anadaiwa Machi 15, jijini Dar es Salaam, alisambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mtoto wa Chacha Wangwe Abadili Msimamo Mahakamani
Mtoto wa Chacha Wangwe Abadili Msimamo Mahakamani
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMWXR5jyYU21WsmdecTsRwL0grh0UUjWb1liS_7u0AdycbKuHK7iXOuqtVR1QP6mktMdwOE-96Cgg32DBA4fRaY8epemd0xvybXfqc27rIyI6aezLIcGRK8DvBZIsoYF4xe5hD0jGvcyjj/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMWXR5jyYU21WsmdecTsRwL0grh0UUjWb1liS_7u0AdycbKuHK7iXOuqtVR1QP6mktMdwOE-96Cgg32DBA4fRaY8epemd0xvybXfqc27rIyI6aezLIcGRK8DvBZIsoYF4xe5hD0jGvcyjj/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/05/mtoto-wa-chacha-wangwe-abadili-msimamo.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/05/mtoto-wa-chacha-wangwe-abadili-msimamo.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy