Tanzania inaungana na Mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (WPFD), ambapo kitaifa maadhimisho ...
Tanzania inaungana na Mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (WPFD), ambapo kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika Jijini Mwanza, ambapo katika kilele cha maadhimisho hayo , Serikali imetakiwa kuharakisha kupitisha Sheria ya Vyombo vya Habari, kwa kuzingatia maoni yanayotokana na mapendekezo ya wadau mbalimbali.
Maadhimisho ya mwaka huu yatakwenda sambamba na matukio muhimu matatu ya kihistoria ya kuadhimisha miaka 250 ya Sheria ya kwanza ya uhuru wa Habari Duniani, ikijumuisha nchi za Sweeden na Finland.
Kumbukumbu nyingine ni miaka 25 ya kupitishwa kwa Azimio la kanuni ya Uhuru wa Hababri ukiwemo mwaka 2016, ambao ni mwaka wa kwanza wa mzunguko wa miaka kumi na tano ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGÃs).
Kutokana na umuhimu wa maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa Taasi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (Misa – Tan) Simon Berege, anazungumzia maandalizi kuelekea kilele cha maadhimisho hayo.
Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, ilianzishwa na Umoja wa Mataifa kusherehekea kanuni za Uhuru wa Habari na kuwakumbuka waliopoteza maisha wakati wakijaribu kutekeleza kanuni hizo.