http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

KIKWETE AZINDUA ZOEZI LA KUPANDISHA MWENGE WA UHURU MLIMA KILIMANJARO KAMA ILIVYOELEKEZWA NA RAIS SAMIA


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Tanzania inapeleka mwenge wa ...

Bodaboda Wapigwa Marufuku Kubeba Wanafunzi na Watoto Chini ya Miaka 10
Tanzia: Balozi Mwambulukutu afariki Dunia
FULL VIDEO: Ripoti ya MCT kuhusu Makonda kuvamia Clouds Media

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Tanzania inapeleka mwenge wa uhuru juu ya mlima Kilimanjaro ili kuitangazia dunia kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni imara na pia itaendelea kulinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Aidha, Waziri Ridhiwani Kikwete amesema kuwa kwa mwaka huu 2024, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamuru mwenge wa uhuru upelekwe juu ya Mlima Kilimanjaro baada ya kuhitimisha mbio zake kwa siku 195.

Mhe. Ridhiwani amesema hayo Oktoba 15, 2024 katika hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro wakati wa hafla ya kupokea kikosi maalumu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambacho kimepewa jukumu la kupeleka Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa la Tanzania kilele cha mlima Kilimanjaro.

Vile vile, Waziri Ridhiwani Kikwete amehamasisha vijana kuendelea kuenzi falsafa za mwenge wa uhuru ulioasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961.

Awali akizungumza, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana amesema kupandishwa mwenge wa uhuru mlima Kilimanjaro mwaka huu 2024 kunaleta hamasa ya uzalendo kwa wananchi hususan wakati huu ambao Tanzania inaadhimisha miaka 60 ya uhuru na mafanikio ya Taifa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia mwenge wa uhuru kupandishwa kwa mara nyingine katika kilele cha mlima Kilimanjaro.

Kwa upande wake, Kiongozi wa hicho Maalum, Luteni Kanali Khalid amemhakikishia Mhe. Waziri Ridhiwani Kikwete kuwa kikosi hicho kitafikisha kinaulinda na kuutunza Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa la Tanzania hadi katika kilele cha mlima Kilimanjaro.


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : KIKWETE AZINDUA ZOEZI LA KUPANDISHA MWENGE WA UHURU MLIMA KILIMANJARO KAMA ILIVYOELEKEZWA NA RAIS SAMIA
KIKWETE AZINDUA ZOEZI LA KUPANDISHA MWENGE WA UHURU MLIMA KILIMANJARO KAMA ILIVYOELEKEZWA NA RAIS SAMIA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWVSuR-ePUsfGbmTZd3djcNDKvyesR2JHZMklFZq0s1YYTjDOqlvuPuSEClCrnj_7W3f3_SVJ50OXPDc6vfyqhNe4yuHvwpF9W7q3Wikb7wcDzEbWZxjn1_lD3icUUx8mivy5bAYqYscJDSUBreD5QTSlyQFctl1Bv0f5EWYKD_JtHI3gtneDw_JFSuTU/s320/IMG-20241016-WA0388-860x573.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWVSuR-ePUsfGbmTZd3djcNDKvyesR2JHZMklFZq0s1YYTjDOqlvuPuSEClCrnj_7W3f3_SVJ50OXPDc6vfyqhNe4yuHvwpF9W7q3Wikb7wcDzEbWZxjn1_lD3icUUx8mivy5bAYqYscJDSUBreD5QTSlyQFctl1Bv0f5EWYKD_JtHI3gtneDw_JFSuTU/s72-c/IMG-20241016-WA0388-860x573.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2024/10/kikwete-azindua-zoezi-la-kupandisha.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2024/10/kikwete-azindua-zoezi-la-kupandisha.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy