Zaidi ya watu 33 wameuwawa katika shambulio jipya lililotokea nchini DRC mauwaji hayo yakihusishwa na fujo za kikabila kati ya jamii ya H...
Zaidi ya watu 33 wameuwawa katika shambulio jipya lililotokea nchini
DRC mauwaji hayo yakihusishwa na fujo za kikabila kati ya jamii ya Hema
na Lendu huko kaskazini Mashariki mwa jimbo la Ituri.
Taarifa
iliyotolewa na radio ya umoja wa mataifa imesema mapigano hayo yaliweza
kudhibitishwa na vyombo vya usalama nchini humo na zaidi ya watu 100
wameuwawa kufuatia vurugu zilizoibuka katika jimbo hilo tangu katikati
ya mwezi Desemba mwaka jana.
Mapigana hayo yaliibuka baada ya jamii ya Hema ambayo ni wafugaji na jamii ya Lendi yenye inajihusisha na ukulima katika jimbo hilo la Ituri ambapo jamii hiyo imeendelea kupigana kwa miaka mingi na kusababisha idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani katika kipindi cha miaka miwili.
Inakadiriwa watu 200,000 wamelazimika kuyakimbia makazi yao kufuatia vurugu hizo katika jimbo hilo la Ituri.