Watu wawili ambao ni wanaondoa wamefariki dunia katika Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha baada ya kuchukuliwa na mafuriko katik...
Watu wawili ambao ni wanaondoa wamefariki dunia katika Wilaya ya
Ngorongoro mkoani Arusha baada ya kuchukuliwa na mafuriko katika mto
Piyaya Kata ya Piyaya wilayani humo.
Picha hii haina uhusiano wowote na habari hii.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Yusuph
Ilembo amesema miili hiyo imeonekana leo majira ya asubuhi baada ya maji
ya mto huo wa msimu kupungua.
Aidha, Kamanda Ilembo amewataja marehemu hao kuwa ni Ormins Sunguyo na mkewe Nembris Sunguyo ambao walikuwa na mtoto wa mdogo aliyefahamika kwa jina la Oloosukuta Sunguyo ambaye alinusurika kifo.
Kamanda Ilembo alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi katika mkoa wa Arusha kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua na kuepuka kuvuka mito wakati maji yanafurika.