http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

WAZAZI WALIOTELEKEZA WATOTO MTAANI KWA KUSHINDWA KUWAJIBIKA KUWALEA KUAWAJIBISHWA

Na Mahmoud Ahmad ARUSHA SERIKALI wilaya ya Arusha, imewataka wazazi ambao wamewatelekeza watoto wao mitaani kwa kushindwa kuwalea kuhakiki...





Na Mahmoud Ahmad ARUSHA
SERIKALI wilaya ya Arusha, imewataka wazazi ambao wamewatelekeza watoto wao mitaani kwa kushindwa kuwalea kuhakikisha wanawajibika kuwaondoa na kuwarejesha majumbani na kuwapatia malezi bora,badala ya kuwaacha waendelee kuishi kwenye mazingira magumu.
Hayo yalielezwa na mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Fabian Daqarro, alipokuwa akifungua mafunzo ya utambulisho wa mfumo wa manegmenti ya kesi za watoto kwa wadau wa huduma ya ulinzi na usalama wa watoto katika jiji la Arusha na wilaya ya Karatu.


Daqarro, alisema katika jiji la Areusha kuna watoto waishio kwenye mazingira magumu na hatarishi wapatao 18834,kutokana na wazazi kutokutimiza wajibu wa kuwalea ,hivyo umefika wakati wazazi lazima wahakikishe wanawaondoa watoto kwenye mazingira hayo hatarishi vinginevyo serikali itawalazimisha.


”Serikali haitaki kuona watoto wanaishi kwenye mazingira magumu na hatarishi huku wazazi wao wapo “‘alisema Daqarro.
alisema haiwezekani wazazi kuwaacha watoto wakihangaika na kutaabika mitaani na kukosa haki zao za msingi zikiwemo elimu, afya,malazi ,lishe bora na upendo, hivyo lazima wahakikishe wanawarejesha majumbani watoto wao.

Aidha, aliupongeza mpango huo ambao umewezesha jiji la Arusha, kuweza kusimamia huduma mbalimbali za watoto kwa kuwa wangelikuwa kwenye hali mbaya kutokana na mazingira waliyokuwa wakiishi.


Ameutaja mpango huo wa Pamoja Tuwalee umesaidia watoto kupata ulinzi ,usalama , afya na kuiwezeshja jamii kutoa mafunzona huduma kwa watoto waishio kwenye mazingira hatarishi.
Aliwataka mganga mkuu wa jiji la Arusha na Idara ya ustawi wa jamii, kuhakikisha wanazingatia matumizi sahihgi ya mfumo huo ili kuepuka kufanya kazi kwa mazoea na kuhakikisha rasilimali zilizopo zinawanufaisha walengwa kwa kutambua wahitaji.


Awali, mkurugenzi wa shirika World Education ,Hindu Ally Mbogo, alisema mpango huo wa Pamoja Tuwalee unafadhiliwa na shirika la misaada la Marekani, USAID, umesaidia kuokoa maisha ya watoto waliopo kwenye mazingira hatarishi.

Alisema mpango huo kuwafikia watoto na kuwapatia huduma mbalimbali ikiwemo kuwapatia elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa taifa wa Pamoja Twaweza Program, Liliani Badi Manara, alisema awamu ya kwanza ya mradi huo inakamilika Novemba 2016


Aidha awamu ya pili ya mradi huo wa miaka mitano unaofadhiliwa na shirika la misaada la Marekani USAID, itatekelezwa na shirika la Pact Tanzania

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : WAZAZI WALIOTELEKEZA WATOTO MTAANI KWA KUSHINDWA KUWAJIBIKA KUWALEA KUAWAJIBISHWA
WAZAZI WALIOTELEKEZA WATOTO MTAANI KWA KUSHINDWA KUWAJIBIKA KUWALEA KUAWAJIBISHWA
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2016/09/Arusha...jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/wazazi-waliotelekeza-watoto-mtaani-kwa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/wazazi-waliotelekeza-watoto-mtaani-kwa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy