diamondplatnumz Laiti ningelikuwa na uwezo ningemuwezesha kila kijana mwenzangu aliyemtaani aweze kupata kazi.....lakini uwezo huo si...
- diamondplatnumz
- Laiti ningelikuwa na uwezo ningemuwezesha kila kijana mwenzangu aliyemtaani aweze kupata kazi.....lakini uwezo huo sina...lakini kwa nafasi ndogo niliyonayo najitahidi kadri ya uwezo wangu, kila niipatapo fursa niitumie vyema kuweza kusaidia na wenzangu...nikiwa miongoni mwa wanamuziki waliopata hatua fani, ninaamini nina deni kubwa kwa Wananchi, Waandishi wa Habari, Watangazaji, Sanaa na hata wasanii wenzangu, Maana naamini uwepo wao ndio Umenifanya niwe hapa...Hiyo ndio sababu kubwa ya mimi kufungua chombo hichi cha @WasafiTv nikiamini kesho na keshokutwa kitakuwa moja ya Mchango wangu katika Tasnia yetu na nchi kwa ujumla... Chombo ambacho kitaongeza Ajira kwa Wanahabari wetu, Watangazaji, Wahitimu wa Shule na Vyuo, Wenye Vipaji na kwapamoja tukashirikiana na Vyombo vyetu vingine vya habari nchini Kupeleka sana na Tamaduni zetu Mbali zaidi..... Mwenyez Mungu Ibariki nchi yetu, ibariki Sanaa yetu na na Vyombo vyetu vyote vya Habari..... Kwakuwa "hii ni Yetu sote"... kabla ya Kuwekea slogani/TagLine tuliyoifikiri...tafadhari wewe tuambie ungependa @wasafiTv itumie Slogan Gani....?