Jeshi la Polisi nchini limevamia mkutano wa Sheikh Issa Ponda ambao ulikuwa unatakiwa kufanyika katika hoteli ya Iris, Kariakoo j...
Jeshi la Polisi nchini limevamia mkutano wa Sheikh Issa Ponda ambao ulikuwa unatakiwa kufanyika katika hoteli ya Iris, Kariakoo jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa amepanga kuzungumzia sakata la Tundu Lissu kupigwa risasi.
Mwenyekiti
wa kamati ya uongozi ya CUF, Julius Mtatiro amethibitisha polisi kuzuia
mkutano huo na kusema kuwa baadhi ya waandishi wa habari ambao
walikuwepo kwenye ukumbi huo wamekamatwa na polisi.
Sheikh Issa Ponda alikwenda kumtembelea, Tundu Lissu hospitali
Nairobi nchini Kenya ambako anapatiwa matibabu kufuatia kushambuliwa kwa
risasi Septemba 7, 2017 mjini Dodoma na baadaye kupelekwa Kenya kwa
matibabu zaidi
"Polisi wamevamia mkutano wa
Sheikh Issa Ponda katika hoteli ya Iris, Kariakoo. Taarifa za awali
zinasema baadhi ya waandishi wamekamatwa. Sheikh Ponda alikuwa azungumze
na vyombo vya habari kuhusu suala la Kupigwa risasi kwa Tundulissu
asubuhi hii, mara baada ya kurejea kutoka Nairobi ambako alizungumza na
Lissu" alisema Mtatiro.