http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Ripoti ya Mtazamo wa Hali ya Haki za Kiraia na Kisiasa Tanzania.........LHRC Wametaja Mikoa 8 hatari kwa kukiuka haki za binadamu


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Kituo cha Sheria na Haki za BInadamu (LHRC) kimetoa Ripoti ya Mtazamo wa Hali ya Kisiasa Tanzania kwa mwaka 2016 ambayo miongoni mwa ma...

Breaking News: IGP Simon Sirro Kaongea na Waandishi wa Habari kwa Mara ya Kwanza na Kutangaza Dau la Milioni 10
Breaking News: Mzee Philemon Ndesamburo(CHADEMA) afariki dunia
Atiwa Mbaroni kwa kutumia nguo za Jeshi la JWTZ kutapeli



Kituo cha Sheria na Haki za BInadamu (LHRC) kimetoa Ripoti ya Mtazamo wa Hali ya Kisiasa Tanzania kwa mwaka 2016 ambayo miongoni mwa mambo mengi yaliyoonyeshwa katika ripo hiyo ni pamoja na mikoa iliyokumbwa na matukio mengi ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Hapa chini ni orodha ya mikoa yenye hatari kwa wakazi wake kutokana na kukiuka haki za binadamu.
Simiyu na Kaskazini Unguja:
Mikoa hii miwili kwa mwaka 2016 imekumbwa na changamoto kubwa katika uhuru wa kujieleza, uhuru wa kukusanyika na haki ya kupiga kura. Lakini kwa upande mwingine mikoa hii imepata alama za juu zaidi katika matokeo ya mtazamo kuhusu haki za kiraia na kisiasa, hasa kwa upande wa haki ya kuishi.
Songwe, Tabora na Shinyanga:
Mikoa hii ilipata alama za chini zaidi ukilinganisha na mikoa mingine yote. Mikoa yote ilikuwa na alama za chini sana kwenye uhuru ya Kukusanyika na haki ya kuishi-mauaji na ukatili mikononi mwa vyombo vya dola. Kama serikali za mikoa zitaendelea kuminya uhuru wa kukusanyika, kushughulikia mauaji yanayotokana na imani za kishirikina na matukio ya kujichukulia sheria mikononi, basi itakua ngumu kupata mwenendo chanya katika mikoa hii.
Morogoro, Arusha na Manyara:
Katika mikoa hii kuna ongezeko kubwa la migogoro ya ardhi ambayo inaweza kupelekea watu kujichukulia sheria mkononi au mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola. Migogoro hii hasa husababishwa na mvutano kati ya wakulima na wafugaji ambapo mara nyingi hupelekea vifo vya raia.
Mbali na mokoa hayo, kituo cha haki za binadamu pia kilitaja haki za raia zilizoongozwa kukiukwa kwa mwaka 2016 ambazo ni pamoja na;
Haki ya Kuishi-Kujichukulia Sheria Mkononi:
Mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro, ambayo kwa sehemu kubwa ni mijini, iliongoza kwa kiasi kikubwa kwenye ukiukwaji wa haki hii. Kuna haja ya polisi na viongozi kurudisha imani ya wananchi juu yao ili kupunguza matuko ya kujichukulia sheria mkononi.
Uhuru wa Kutoa Maoni:
Athari ya Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari zitakuwa ni za muhimu sana kufanyiwa uchambuzi kwa mwaka 2017 hasa kwa kuwa uhuru wa vyombo vya habari umeelezwa kuwa miongoni mwa matatizo katika mikoa iliyopata alama za chini.


Ukizingatia shinikizo ndani nan je ya nchi, itakuwa muhimu kuangalia kama Serikali itayafanyia kazi mapendekezo ya watetezi wa haki za 21 Matukio Makubwa yaliyotokea Mwaka 2016 Mtazamo wa Haki za Kiraia na Kisiasa 2016 Mikoa na Haki za Kuangalia mwaka 2017 Methodologia na Alama binadamu ya kurekebisha vipengele vya sheria hiyo vinavyominya haki.
Uhuru wa Kukusanyika:
Tumeshuhudia zuio la mikutano na mikusanyiko ya kisiasa kwa mwaka 2016, kitendo ambacho kimepelekea mtazamo kwamba uhuru wa kukusanyika imeminywa. Japokuwa Jeshi la Polisi baadae liliondoa zuio hilo, kitendo hicho kiliendelea kuathiri mtazamo kuhusu uhuru wa kukusanyika.
Haki ya Kuishi – Mauaji na Ukatili Mikononi mwa na Vyombo vya Dola:
Matukio ya mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola yamechangia kwa kiasi kikubwa kushusha alama za haki katika mikoa mingi.


Japokuwa kumekuwa na ongezeko la mashtaka ya mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola, ikiwemo askari polisi wawili kukutwa na hatia ya mauaji hivi karibuni, kauli na matamko mbalimbali za viongozi wa serikali ambayo yanaweza kuchochea mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola yanaweza kuwa chanzo cha mauaji pia.
Unaweza kupakua ripoti nzima hapa chini;

Ripoti ya Mtazamo wa Hali ya Haki za Kiraia na Kisiasa Tanzania

The Tanzania Civil and Political Rights Perceptions Index

source....mpekuzihuru

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Ripoti ya Mtazamo wa Hali ya Haki za Kiraia na Kisiasa Tanzania.........LHRC Wametaja Mikoa 8 hatari kwa kukiuka haki za binadamu
Ripoti ya Mtazamo wa Hali ya Haki za Kiraia na Kisiasa Tanzania.........LHRC Wametaja Mikoa 8 hatari kwa kukiuka haki za binadamu
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEginw_eDF8W7yFOREe0cr-LF7brACjicRwItepz851vHE7OvEEc2guPfUMO3aheVBgo7C7AH_0sOixCm6uZgreX1PZDsoxQL8UPXzTxh9ISckgE8FcibJTRRgk8CNmIT8AIbdqFwHIH9wY/s640/1.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEginw_eDF8W7yFOREe0cr-LF7brACjicRwItepz851vHE7OvEEc2guPfUMO3aheVBgo7C7AH_0sOixCm6uZgreX1PZDsoxQL8UPXzTxh9ISckgE8FcibJTRRgk8CNmIT8AIbdqFwHIH9wY/s72-c/1.png
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/12/ripoti-ya-mtazamo-wa-hali-ya-haki-za.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/12/ripoti-ya-mtazamo-wa-hali-ya-haki-za.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy