BWANA YESU asifiwe. Ninamtukuza Mungu kwa upendeleo alionipa hata nikaiona siku ya leo, kwa maana sikufanya jambo jema ambalo lingeni...
BWANA YESU asifiwe.
Ninamtukuza Mungu kwa upendeleo alionipa hata nikaiona siku ya leo, kwa maana sikufanya jambo jema ambalo lingenifanya nifike siku ya leo.
Atukuzwe Mungu anayetuwazia mema kila iitwapo leo
kijana ndiye taifa la leo na pia taifa la kesho kwa siku ya leo tuangazie sifa za kijana anayefaa kuwa mke ama mume katika maisha ya ndoa. tukianza na sifa ya kwanza kabisa ambayo ni kubwa na yenye matokeo makubwa kwenye maisha ya kila mwaanadamu.
1. HOFU YA MUNGU.
Hofu ya Mungu ni nini? Watu wengi hudhani kuwa, kuwa na HOFU YA MUNGU ni kuhubiri, kuimba kwaya, kushuhudia nyumba kwa nyumba, kutoa sadaka, kukemea mapepo, kuhudhuria ibadani, N.K, kitu ambacho siyo kweli.
Kutokana na dhana walizonazo watu wengi katika vichwa vyao huwapelekea kufanya vitu ambavyo kimsingi havina faida yoyote kwao.
Unakuta mtu anahubiri, anafunga, anaomba, anaimba kwaya, anatoa sadaka, N.K, lakini ndani ya moyo wake anashuhudiwa kabisa kuwa yeye ni mpagani/haishi sawasawa na Neno la Mungu.
Kutokana na kutokuwa na HOFU YA MUNGU na kujiepusha na uovu mtu huyo anafanya kazi ya bure (kazi isiyo na faida),
Imeandikwa “Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali name, Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu” MATHAYO 15:8-9.
Hofu ya Mungu ni hali ya utii na unyenyekevu aliyonayo mtu ndani ya moyo wake.
Hali hiyo humpelekea mtu kuishi sawasawa na Maagizo ya Mungu/Neno la Mungu.
Yaani HOFU YA MUNGU humfanya mtu kuyajua yale yampasayo kutenda na yasiyompasa kutenda.
HOFU YA MUNGU humfanya mtu kuishi MAISHA HALISI, Yaani kutokuishi maisha ya maigizo.
Mtu aliye na HOFU YA MUNGU kila jambo analolifanya ni halisi kwake, ikiwa ni kutumika mbele za Mungu ni kiuhalisia, anapofanya ibada mbele za Mungu ni ibada halisi. YOHANA 4:23-24.
Hafanyi jambo kwa kufuata mkumbo tu, kama wasio na HOFU YA MUNGU wafanyavyo,
kijana yeyote mwenye hofu ya Mungu awe wakike ama wakiume katika ndoa ataishi kwa amani na ndoa yakudumu.
2. UNYENYEKEVU
Unyenyekevu ni nini?
Mika 6:8 “Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!”
Unyenyekevu ni hali ya kukubali kuwa chini ya uongozi wa Mungu, kumtegemea yeye na kujiona kuwa hauwezi kitu bila msaada wake. Ni hali ya kuwa tayari kuwasikiliza na kuchukuliana na wengine hata kama unaona umewazidi kila kitu. Unyenyekevu sio kujiona hufai mbele za wengine bali ni hali ya kutokuwa na kiburi wala dharau.Mtu mnyeyekevu hatumainii nguvu au uwezo wake bali anatumainia uwezo wa Mungu.
Ukiwa mnyenyekevu hautakuwa na sababu ya kupingana na kugombana na aliye kuudhi maana unajua nafasi yako mbele za Mungu na utarudi kwa Mungu ili kupata hekima za kukabiliana na jambo husika, Mithali 11:2 “Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu bali hekima hukaa na wanyenyekevu”. Uyenyekevu utakufanya uwe na pendo la Mungu na kuwatayari kuwatanguliza wengine katika mambo yote, wafilipi 2:3 “Msitende neno lolote kwa kushindana wala majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwengine kuwa ni bora kuliko yeye”.
Hali ya unyenyekevu umfanya mtu kuwa na utu wema na ufaa kuwa mke au mme kwa kigezo hicho.
3. KUJITOA NA KUJITUMA
Hali ya mtu kujitoa na kujituma kwa mambo yake mwenyewe utampelekea kwenye njia ya mafanikio katika maisha yake na kazi ya mikono yake, mtu akiwa mvivu hata siku moja hatakuwa na hali yakujituma na kujitoa popote pale
hali ya kijana wakike au wakiume kuwa na moyo wakufanya jambo kwa kutokutanguliza pesa ama jambo lolote ni hali yakujitoa
BY RAYMOND WILLIAM
ITAENDELEA.................................................