http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo kuanzia jana.  Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi w...

Msimamo wa Rais Magufuli Kuhusu Katiba Mpya Wamtesa Tundu Lissu
Waliokula Fedha za Mikopo Elimu ya Juu Kitanzini....Sheria Yarekebishwa Kuwabana Zaidi
Watu 17 Mkoani Shinyanya wamefariki Dunia kwa Ajali......
Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo kuanzia jana. 
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa ikimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema Rais amemteua Dk Charles Mlingwa ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Siha kujaza nafasi hiyo. 
Mulongo anakuwa mkuu wa mkoa wa pili kutimuliwa kazi na Rais Magufuli baada ya Anne Kilango Malecela aliyekuwa Shinyanga.

Hata hivyo, tofauti na Kilango ambaye alitimuliwa kutokana na kutoa taarifa potofu kuhusu watumishi hewa mkoani mwake, Ikulu haikutoa sababu za kutenguliwa kwa uteuzi wa Mulongo.

Mulongo ameondolewa madarakani miezi sita baada ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Dk Faisal Issa baada ya kutofautiana na Mulongo wakati huo akiwa mkuu wa mkoa huo.

Baada ya kumwondoa Dk Issa na nafasi yake kujazwa na aliyekuwa Kamishna wa Polisi, Fedha na Utawala (CP) Clodwig Mtweve, miezi miwili baadaye Rais alimbadilisha Mulongo kituo cha kazi akimhamishia Mara.

Alipoulizwa jana jinsi alivyoipokea hatua hiyo iliyochukuliwa dhidi yake Mulongo alisema: “Sina taarifa rasmi.” 

Kabla kuhamishiwa Mara akitokea Mwanza, Mulongo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Alishika nafasi hiyo baada ya kupandishwa cheo akiwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo
Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdOyUV3lSmwwGJXb9bH3JV9XuUITYb9fJpCJLaoizzjMRRFyb-lnJOS2jNAoeEMmRY_Lev1yez_HeJdLDMkFBhnIwCgUgu39RNfq9phEzFslw2VozkJF3CEsIYq1A29UiB1QZzS6r2aEQ/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdOyUV3lSmwwGJXb9bH3JV9XuUITYb9fJpCJLaoizzjMRRFyb-lnJOS2jNAoeEMmRY_Lev1yez_HeJdLDMkFBhnIwCgUgu39RNfq9phEzFslw2VozkJF3CEsIYq1A29UiB1QZzS6r2aEQ/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/06/rais-magufuli-atengua-uteuzi-wa-mkuu-wa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/06/rais-magufuli-atengua-uteuzi-wa-mkuu-wa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy