http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Zitto Kabwe: Watanzania wakifa njaa Tutaiwajibisha Serikali kwa mujibu wa Katiba ibara ya 46A

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema endapo Mtanzania yeyote atakufa kwa njaa watachukua jukumu la kumwajibisha Rais kwa kusema wa...


Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema endapo Mtanzania yeyote atakufa kwa njaa watachukua jukumu la kumwajibisha Rais kwa kusema waziwazi kwamba hajatimiza wajibu wake.


Akihutubia mkutano wa kampeni katika Kata ya Kijichi jana, kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto alisema, “Tunamkumbusha Rais kwamba kwa mujibu wa ibara ya 46A ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo yeye amekula kiapo kuilinda, kuihifadhi na kuitetea, Bunge laweza kumshtaki kwa kosa la mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais. "


Kauli hiyo ya Zitto ilitokana na msimamo wa Rais Magufuli kuwa hakuna njaa nchini na kwamba Serikali haitatoa chakula cha msaada, huku makundi mengine ya wananchi, wakiwamo wanasiasa na viongozi wa dini wakisema kuna upungufu wa chakula uliotokana na ukame.


Zitto ambaye kabla ya kuhutubia alipita nyumba za jirani na uwanja akisalimia, alisema, “Tumesema hili la njaa katika kutekeleza wajibu wetu, Rais na Serikali wamejibu na kufunga mjadala. Wakati utaamua na kuonyesha mkweli nani na mpiga propaganda nani.”


“Tunamwambia Rais kwamba, Mtanzania yeyote akifa kwa njaa kwa sababu Serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake, Watanzania tutapaswa kuchukua hatua, Katiba inatulazimisha kumtoa Rais madarakani.


“Jambo moja ni muhimu sana, Rais anapaswa kujua kuwa anafanya kazi kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Na Katiba imetoa wajibu wa lazima kwa Serikali kulinda watu. Ndio kazi ya Serikali – kulinda wananchi pale ambapo yanatokea majanga ambayo yanazidi kimo wananchi hao,” aliongeza.


Alisema Rais yupo chini ya Katiba na kwa idadi ya wabunge wa upinzani waliopo bungeni, na wakiamua kusimama na wananchi kulinda Katiba, anaweza kuwa wa kwanza wa nchi yetu kutolewa hoja ya kutokuwa na imani naye bungeni.


“Katiba inahitaji asilimia 20 tu ya wabunge kuwasilisha hoja hiyo bungeni,” alisema.


Mbunge huyo alitoa wito kwa Watanzania bila kujali vyama vyao, kuweka rekodi ya hali ya chakula popote walipo na kuweka takwimu ya maafa yeyote yanayotokana na njaa.


Alimtaka Rais atumie lugha ya kujenga matumaini badala ya kujenga hofu kwenye jamii, aache kuonea watu kwa kutumia madaraka yake, na akumbuke cheo ni dhamana.


Kiongozi huyo alisema ameamua kusema hayo kwa sababu baada ya siku saba hawatakuwa na nafasi ya kuzungumza majukwaani kama viongozi wa vyama vya siasa kwa sababu ya zuio lisilo la kikatiba la kuzuia mikutano ya hadhara.


Hata hivyo, sheria inasema janga la njaa linaweza kutangazwa na Rais tu na si mtu mwingine.
Advertisement


Credity ...Mpekuziblog

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Zitto Kabwe: Watanzania wakifa njaa Tutaiwajibisha Serikali kwa mujibu wa Katiba ibara ya 46A
Zitto Kabwe: Watanzania wakifa njaa Tutaiwajibisha Serikali kwa mujibu wa Katiba ibara ya 46A
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh2sYJDBRIoPmUMCyH0aq2SshiFBY_3ig5fVPtBTHpXmZgJxsf-T8yXzxCiVKPfT-6mh7L2y9DKhrtt7IZt6FSaMIGl-LdIr6ibwwglju6osPjuUsHOz9Nb5ZoyDW4wYJamytGoSRLjPpI/s1600/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh2sYJDBRIoPmUMCyH0aq2SshiFBY_3ig5fVPtBTHpXmZgJxsf-T8yXzxCiVKPfT-6mh7L2y9DKhrtt7IZt6FSaMIGl-LdIr6ibwwglju6osPjuUsHOz9Nb5ZoyDW4wYJamytGoSRLjPpI/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/01/zitto-kabwe-watanzania-wakifa-njaa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/01/zitto-kabwe-watanzania-wakifa-njaa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy