Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda akizungumza na Wagonjwa katika Hospitali ya Ngarenaro iliyoko jijini Arusha ,hospitali hiyo in...
Hospitali
ya Ngarenaro inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya kuhudumia wagonjwa
pamoja na kukosekana kwa miundombinu imara ya maji katika chumba cha
upasuaji hivyo kuhitaji upanuzi pamoja na ukarabati wa hospitali hiyo
ambayo inahudumia zaidi ya Wakazi 74000 wa kata ya Ngarenaro jijini
Arusha.
Akizungumzia
changamoto hizo Daktari Mfawidhi wa Hospitali hiyo Josephat Kivuyo
katika taarifa yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Kivuyo amesema kuwa
hospitali hiyo inahitaji upanuzi na ukarabati ili kuweza kuboresha
huduma za afya ambazo zinahitajika na wananchi wengi.
Daktari
huyo Mfawidhi alisema kuwa changamoto nyingine ni uhaba wa magari ya
wagonjwa maarufu kama Ambulance kwani gari lililopo ni la zamani na
haliwezi kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kama inavyotarajiwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda amewataka wananchi na wadau
mbalimbali kuunganisha nguvu katika kuboresha huduma kwa kufanya
ukarabati ambao tayari umeshaanza ili kuboresha mazingira bora kwa
wananchi na wahudumu wa afya.
Pia
Amewataka Wahudumu wa Afya kuepuka kutoa lugha mbaya kwa wagonjwa na
kuwahudumia vizuri ili kupunguza malalamiko katika sekta ya afya ambayo
inahudumia watanzania wengi.
Alisema
Ukarabati wa Kituo cha Afya cha Ngarenaro unaendelea na tayari hivyo
nguvu ya serikali n wadau wa maendeleo inahitajika katika kuhakikisha
kuwa vituo hivi vinakuwa katika mazingira rafiki ya utoaji huduma za
afya.
Na Woinde Shizza,Arusha.