Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda leo Oktoba 15, 2024 amelazimika kutumia usafiri wa pikipiki na bajaji kuham...
Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda leo
Oktoba 15, 2024 amelazimika kutumia usafiri wa pikipiki na bajaji
kuhamasisha wananchi wa Wilaya ya Babati kujitokeza kushiriki
kujiandikisha na kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa
unaotarajia kufanyika Novemba 27, 2024.
Mhe.
Kaganda akiwa kwenye bajaji alizunguka maeneo kadhaa ya mji wa Babati
ikiwa ni pamoja na kwenye vituo vya maafisa usafirishaji (bodaboda) na
maeneo ya Wamachinga na mama lishe kuwaambia umuhimu wa kujiandikisha
kwenye daftari hilo la makazi kwa ajili ya kuchagua wenyeviti wa
Mitaa,vijiji na vitongoji.
Kaganda ambaye naye amejiandikisha katika mtaa wake wa Mrara Mjini
Babati amesema zoezi hilo linatumia dakika Moja Hadi mbili kukamilika na
kwamba hakuna chochote anapaswa kwenda nacho mtu kituoni , "kikubwa ni
kutaja majina yako matatu na kuweka Saini inakuwa umemaliza" alisema
Kaganda
Baadhi ya Wakazi wa mji wa Babati wamempongeza mkuu wa wilaya kwa
uhamasishaji huo anaoendelea kuufanya kwa kuwa unawapa msukumo watu
kwenda kujiandikisha kwani wengi wao walikuwa wakiufananisha mchakato
huo na ule uliopita wa kujiandikisha kwenye daftari la Kudumu la wapiga
kura linalosimamiwa na tume huru ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi ujao
wa madiwani,wabunge na Rais.
Mwenyekiti wa boda
boda mkoa wa Manyara Adamu Omari, amesema wataendelea kuhasishana
wenyewe kwa wenyewe kwenye vijiwe vyao kwenda kujiandikisha.
Zoezi hilo la kujiandikisha litadumu hadi Oktoba 20,2024 na halina marudio.