Polisi Mkoa wa Arusha wamemuua kwa kumpiga risasi jambazi sugu aliyekuwa akisakwa kwa muda mrefu kuhusiana na matukio ya uporaji wa kutumia ...

Polisi Mkoa wa Arusha wamemuua kwa kumpiga risasi jambazi sugu aliyekuwa akisakwa kwa muda mrefu kuhusiana na matukio ya uporaji wa kutumia silaha wakati akijiandaa kufanya tukio la uporaji
Akizungumza na waandishi wa habari mapema Leo,Juni 5 ofisini kwake ,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng'anzi alisema mtu huyo ambaye anadaiwa kuwa ni jambazi sugu alitambulika kwa jina moja la Riziki mwenye umri wa miaka kati ya (20 na 25) aliuawa katika mapambano ya risasi na polisi
Amesema jambazi huyo aliuliwa majira ya saa 12:00 jioni katika eneo la stendi ya mabasi madogo ya Kilombero baada ya Polisi kupata taarifa za kiintelijensia kuhusu uwepo wa jambazi huyo akijiandaa kwenda kufanya tukio na e kwenye moja ya kituo cha kuuzia mafuta kilichopo Jijini hapa.
Alisema baada ya polisi kupokea taraifa hiyo askari walikwenda eneo la tukio kwa lengo la kumkamata na mara baada ya kuwaona askari jambazi huyo alitoa silaha yake aina ya bastola aliyeificha kiunoni na kuanza kurusha risasi kwa nia ya kuwalenga askari waliokuwa wanataka kumkamata .
Aliongeza kuwa risasi moja ilimjeruhi mpita njia aitwaye Halima Salim(20) Mkazi wa Arusha kwenye mguu wake wa kulia na anaendelea na matibabu hospitali ya Mount Meru.
Alisema baada ya jambazi huyo kumjeruhi mpita njia huyo askari
walijibu mapigo kwa kupiga risasi moja ambayo ilimjeruhi juu ya tumbo
na kufariki dunia wakati akipelekwa hospitali ya Mount meru na
kusongeza kuwa marehemu alikutwa akiwa na silaha aina Chinese
iliyofutwa namba ikiwa na risasi tatu kwenye magazine na kwenye eneo
kulikutwa maganda mawili ya risasi.
Wakati huo huo, Mnamo Juni 4 mwaka huu saa 1:00 jioni katika eneo la
Ngaresero kata ya Usa River mtu mmoja wa kiume ambaye hakufahamika
jina anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 28 hadi 30 alikutwa amekufa
pembezoni mwa barabara huku mwili wake ukiwa na jeraha kichwani
lililotokana na kuchomwa na kitu chenye ncha kali.
Kamnada Ng'anzi alisema chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika na
polisi wanaendelea na upelelezi huku mwili wake ukiwa umehifadhiwa katika hospital ya Mkoa Mount Meru



