Rais wa Jamnhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Siza Donald Tumbo kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Utawala...

Rais wa Jamnhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Siza Donald Tumbo kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Utawala ya Chuo cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College).
Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa imesema kuwa uteuzi huo umeanza rasmi leo Mei 13.
Kabla ya uteuzi wa leo Prof Tumbo alikuwa Mkurugenzi Mkuu
wa Kituo cha zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (Center for
Agriculture Mechanization and Rural Technology - CAMARTEC).
Wakati huo huo Rais Magufuli amemteua Mhandisi Mussa Iyombe
kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi
wa Umma.




