Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeadhimia kuligawa Jimbo la Mbagala liliopo Jijini Dar ...

Serikali
kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
imeadhimia kuligawa Jimbo la Mbagala liliopo Jijini Dar es Salaam baada
ya kuwepo kwa idadi kubwa ya wakazi wanaoishi jimboni humo na
kusababisha uhaba wa upatikaji wa huduma za muhimu kutoka kwa Mbunge
wao.
Kauli
hiyo imetolewa leo Mei 11, 2018 na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph Kakunda Bungeni Jijini
Dodoma kwenye kikao cha 27 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la nyongeza la Mbunge Mariam
Kisangi aliyetaka kujua serikali inamkakati gani wa kuligawanya Jimbo la
Mbagala ili liweze kufikika kiurahisi na hata Mbunge wao aweze kutoa
kwa wananchi kwa wakati.
"Ni
kweli Jimbo la Mbagala kwa idadi ya watu ni miongoni mwa majimbo yenye
watu wengi zaidi hasa ya Dar es Salaam, lakini hivi karibuni tumeyagawa
majimbo ya jiji hilo.
"Kwa
hiyo mimi nilikuwa nashauri kwa vigezo vile ambavyo nimevizungumza
katika majibu ya msingi, ninaomba sasa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
wakae na waweze kupendekeza na mwishowe wapeleke mapendekezo yao moja
kwa moja katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)", amesema Kakunda.
Kwa
mujibu wa Mbunge Mariam Kisangi amesema Jimbo la Mbagala mpaka hivi
sasa lina jumla ya wananchi Milioni moja na laki moja jambo ambalo
linapelekea utoaji wa huduma kuwa mgumu pamoja na kuharibika kwa
miundombinu mara kwa mara kutokana na wingi wa watu waliopo jimboni
humo.



