http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Wanafunzi 400 wavamia Nyumba ya Mwalimu na Kufanya Vurugu....Shule Yafungwa Wiki 2

Serikali imeifunga Shule ya Sekondari ya Lyamungo iliyoko Hai mkoani Kilimanjaro, baada ya wanafunzi wake kuzusha vurugu kubwa huku wak...

Serikali imeifunga Shule ya Sekondari ya Lyamungo iliyoko Hai mkoani Kilimanjaro, baada ya wanafunzi wake kuzusha vurugu kubwa huku wakivamia na kuivunja ofisi ya Makamu Mkuu wa shule hiyo.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Hai, Onesmo Buswelu, alithibitisha jana kuifunga sekondari hiyo ya kitaifa kuanzia Machi Mosi hadi Machi 17, mwaka huu.

Shule hiyo ya kitaifa hupokea wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita kutoka mikoa mbalimbali nchini.

"Ni kweli nimeifunga hiyo shule kwa zaidi ya wiki mbili kutokana na sababu za kiusalama. kulikuwa na uchaguzi wa serikali ya wanafunzi na wakati unafanyika mwanafunzi mmoja aliandika matusi makubwa akiwatukana walimu.

"Baada ya kufanyika uchunguzi aligundulika huyo mwanafunzi na hapo ndiko walipoandaa vurugu hizo na kujielekeza kuharibu mali na kusababisha hasara ambayo bado haijafahamika," alisema Buswelu.

Kwa mujibu wa Buswelu, vurugu hizo ziliibuka baada ya mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) kupewa barua ya kufukuzwa shule kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu.

Buswelu ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Siha ameagiza Bodi ya shule hiyo kukutana kesho (leo) kufanya tathmini ya hali ya uharibifu na madhara yaliyojitokeza na kuiarifu serikali.

Mpaka sasa, hakuna mwanafunzi anayeshikiliwa kwa kufanya vurugu na kusababisha hasara ya mali na rasilimali za serikali.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Hamisi Issah, alisema wanafunzi hao walifanya tukio hilo saa 4:30 asiku juzi.

"Hao wanafunzi wameharibu ofisi ya mwalimu huyo ambaye pia ni mwalimu wa nidhamu kwa kuvunja paa la juu, milango, madirisha na samani za ndani," alisema Kamanda Issah.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Wanafunzi 400 wavamia Nyumba ya Mwalimu na Kufanya Vurugu....Shule Yafungwa Wiki 2
Wanafunzi 400 wavamia Nyumba ya Mwalimu na Kufanya Vurugu....Shule Yafungwa Wiki 2
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgdiizGKYn_ot3U_vdPKBDQbL-GKSE4h_98BeYulF-8rgYowVwFJH9ameV6LAChacxkUAVQ9gt1f8vvFn4UdIf5ed1dOlpt2m2Q0ihBsVA_kitutizfP2KVHio-m5U1Nye5DAwnMyLhckA/s1600/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgdiizGKYn_ot3U_vdPKBDQbL-GKSE4h_98BeYulF-8rgYowVwFJH9ameV6LAChacxkUAVQ9gt1f8vvFn4UdIf5ed1dOlpt2m2Q0ihBsVA_kitutizfP2KVHio-m5U1Nye5DAwnMyLhckA/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2018/03/wanafunzi-400-wavamia-nyumba-ya-mwalimu.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2018/03/wanafunzi-400-wavamia-nyumba-ya-mwalimu.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy