Serikali ya mkoa wa Mbeya kupitia Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Mariam A. Mtunguja imetangaza kuanza leo Februari 28 zoezi la kuhakiki upya...
Serikali ya mkoa wa Mbeya kupitia Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Mariam A.
Mtunguja imetangaza kuanza leo Februari 28 zoezi la kuhakiki upya vyeti
vya kidato cha nne na sita kwa watumishi wake, kufuatia kupata taarifa
uwepo watumishi ambao wanavyeti feki
Taarifa
ya Katibu Tawala imesema kuwa wameamua kurudia zoezi hilo la kuhakiki
upya vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita ili kuwabaini watu
ambao bado wananufaika na malipo ya serikali licha ya kuwa na vyeti
feki.





