Wabunge na Madiwani wa Chadema, leo mchana Machi 29, 2018 wameandamana kwenda ofisi za Umoja wa Ulaya (EU). Wabunge hao wamekwenda k...

Wabunge hao wamekwenda katika ofisi hizo kulalamikia kile wanachofanyiwa viongozi sita wa chama hicho akiwamo mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe waliopo mahabusu.
Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema, “Tuko EU (Umoja wa Ulaya). Tupo
wabunge wote tumeandamana kuja hapa kuleta kilio chetu.”
Miongoni
mwa Viongozi waliofika katika ubalozi huo ni Mbunge wa Arusha Mjini
Godbless Lema, Meya wa Ubungo Bonface Jacob ambapo wametahadhalisha
usalama wa Viongozi hao pamoja wafuasi wa chama hicho.





