waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo Dk Harison Mwakyembe, akizungumza katika ufumbuzi wa kikao Kikao kazi ya 14 cha maafisa haba...
![]() |
| waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo Dk Harison Mwakyembe, akizungumza katika ufumbuzi wa kikao Kikao kazi ya 14 cha maafisa habari, mawasiliano na uhusiano serikalini |
NA RAYMOND WILLIAM
Kikao kazi ya 14 cha maafisa habari, mawasiliano na uhusiano serikalini lenye lengo la kuwapa maafisa habari uwezo wakuyasemea yale yanayotendwa na serikali ya Tanzania katika awamu ya 5 inayo ongozwa na Dk John Magufuli, Imeanza siku ya leo jijini Arusha.
Kikao hicho ambacho kitadumu ndani ya siku 5, kuanzia leo 12/3/2018 mpaka 16/3/2018 ambapo kikao hicho kimefunguliwa na mgeni rasmi waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo Dk Harison Mwakiymbe.
Akitoa hotuba ya ufumbuzi wa kikao hicho Mwakyembe amewataka maafisa habari kuuwisha tovuti za halmashauri kwa kuweka habari zinazotokana na Halmashauri zao ikiwa na lengo la kuongeza uwezo wa serikali kuipatia jamii habari kwa haraka.
Ameongeza kwa kuwataka mahafisa habari kutogeuza tovuti hizo kuwa magofu ya habari badala yake wafanye yawe majokofu ya taarifa ya habari kwa wanajamii wao wanao wazunguka
“Lengo la mradi wa tovuti kitaifa kuongeza uwezo wa serikali kuwapatia wananchi Habari na taarifa kwa haraka, tuko katika kipindi muhimu ya mageuzi katika historia ya nchi yetu, amabpo mengi yanafanyika serikalini kiuchumi na kijamii, lakini hayaelezwi. Tovuti zifanye kazi hiyo, Maafisa habari mmesomea uandishi wa habari wekeni habari na taarifa kwa njia ya picha mnato, picha jongevu maandishi na hata kwa sauti na ziwe fupi fupi ili watu waamasike kutazama au kutembelea tovuti zenu mara kwa mara. Tovuti hizi zisigeuke kuwa Magofu ya habari bali ziwe majokofu ya habari”
![]() |
| waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo Dk Harison Mwakyembe, akizungumza katika ufumbuzi wa kikao Kikao kazi ya 14 cha maafisa habari, mawasiliano na uhusiano serikalini |
Mwakiymbe amezitaja halmashauri zinazofanya vizuri katika kuhuwisha tovuti zao kwa kuweka taarifa zinazotokana na halmashauri zao ni jumla ya Halmashauri tisa: Kishapu, Mtwara ,mikindani, Mufindi, Mlele katavi, Kinondoni, Ilala, Ubungo na Kibaha.
Pia amezitaja mikoa ambazo zinafanya vizuri zaidi katika kuhuwisha taarifa zao katika tovuti ikiwa ni Mwanza, Mara, Kagera, Tabora, Shinyanga, Simiyu, Arusha, Tanga, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Iringa, Morogoro, Geita, Katavi na Songwe.
Hataivyo amekiri kuwepo kwa tatizo kubwa kwa upande wa baadhi ya viongozi ya kutokuona umuhimu wa mawasiliano yakaribu na uma ndiyo maana halmashauri nyingi azina maafisa habari na akuna anae jali na kuwepo kwa maafisa walioshikilia nafasi hizo huku awana taaluma hiyo na wengine wapo lakini awatambuliki kama wapo na wanaumuhimu wao.





