Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kuanzia usiku wa jana Machi 1, 2018 hadi leo Machi 2, 2018 kutakuwa na vipindi vya m...

Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kuanzia usiku wa jana Machi 1,
2018 hadi leo Machi 2, 2018 kutakuwa na vipindi vya mvua kubwa katika
maeneo mengi ya nyanda za Juu Kaskazini Mashariki.
Taarifa
ya TMA iliyotolewa imebainisha maeneo hayo kuwa ni mikoa ya Arusha,
Manyara na Kilimanjaro ambapo mvua hizo itazidi milimita 50 ndani ya saa
24 huku ilieleza hali hiyo inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua.
TMA
imewashauriwa wakazi wa maeneo husika kuchukua tahadhari stahiki na
kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zinazotolewa.



