Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amejitosa sakata maandamano linalosambaa katika mitandao ya kijamii, kwa kuwaonya...

Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amejitosa sakata
maandamano linalosambaa katika mitandao ya kijamii, kwa kuwaonya
wanaotishia kuandamana kwa kusema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama viko
imara.
Masauni
ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Machi 15, jijini Dar es Salaam wakati
akipokea vituo sita vya polisi vinavyohamishika vilivyotolewa na kampuni
ya vinywaji baridi ya Coca-Cola kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi
Kinondoni.
“Kuna
watu wako ndani ya nchi na wengine nje ya nchi wanaotaka kukwamisha
ajenda ya maendeleo watupeleke kwenye ajenda zisizo za msingi.
“Utasikia
mwingine anasingizia polisi kuwa katekwa kumbe kajiteka mwenyewe,
mwingine anataka watu waandamane, yaani watu waache kutumia fursa
zilizopo kwa mfano jana Rais kazindua reli ya umeme ambayo mimi nilikuwa
naiona Ulaya leo inajengwa Tanzania, waache kutumia fursa za viwanda
vinavyoibuka kwa wingi kama uyoga eti wakaandamane.
“Ninachoweza kuwahahikikishia ni kwamba vyombo vyetu viko imara,” amesema Masauni.



