Jeshi la Polisi limezitaka Kampuni binafsi za ulinzi hapa nchini kuvaa sare za aina moja ifikapo Januari 1, 2019 kwa lengo la kuondoa sa...
Jeshi la Polisi limezitaka Kampuni binafsi za ulinzi hapa
nchini kuvaa sare za aina moja ifikapo Januari 1, 2019 kwa lengo la
kuondoa sare ambazo zimekuwa zikifanana na zinazovaliwa na Askari wa
Vyombo vya Ulinzi na Usalama
-
Sare zilizokubaliwa kwa pamoja kati ya Jeshi la Polisi na wawakilishi wa kampuni binafsi za ulinzi zinatakiwa ziwe na rangi ya bluu nyeusi(Dark blue), nyeusi pamoja na mashati meupe kulingana na mazingira ya kampuni inapofanyia ulinzi
-
Agizo hilo limetolewa na Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii, Mussa Alli Mussa baada ya kukamilika kwa kikao kilichowakutanisha wamiliki wa kampuni binafsi za ulinzi
-
Katibu wa Chama cha wamiliki wa kampuni binafsi za ulinzi(TAPSCOA), Shawiniaufoo Kimuto amesema jambo hilo litasaidia kufahamika kwa urahisi kwa walinzi wa kampuni binafsi na hivyo kuwa rahisi kupata msaada pindi wanapotekeleza majukumu yao