http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Familia yatoa neno kupotea Abdul Nondo

Familia ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (U...

Familia ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) imefunguka na kuwataka watu ambao wamemteka mwanafunzi huyo kuhakikisha anamrejesha akiwa mzima.
Baba mdogo wa Abdul Nondo amesema hayo leo Machi 7, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari kipindi ambacho viongozi wa mtandao huo wa wanafunzi wakitoa rai yao kwa jeshi la polisi kuhusu kupotea kwa mwenzao.
"Abdul ni kijana mdogo mno na amewahi kutuambia mara kwa mara kuhusu vitisho ambavyo amekuwa akivipata lakini hatuna nguvu kusema kuwa tutamkinga vipi. Sisi kama familia tunaomba kijana arudi akiwa mzima maana ana ndoto zake, mama yake saizi mgonjwa anaumwa pressure baba yake pia. Huyu Nondo ana ndoto zake kama mtoto pia ana ndoto zake kama mwanafunzi atatimiza vipi, sisi kama familia bado tunaendelea kulaani na tunavuta subira katika hili kwamba huenda akapatikana tunachoomba aje salama asije akarudi hana mkono akashindwa kusonga na kumsaidia mama yake" alisema baba mdogo wa Abdul
Baba mdogo wa Abdul aliendelea kusema
"Hatujui alipo lakini kama yupo kwa wale ambao tunawasikia kila siku maanake wanajulikana tunaomba arudi huyu kijana maisha yake na historia yake ni ngumu wamrudishe huyu kijana anatafuta njia hana kingine anachokitafuta pale, kuongea sana vile au kujionyesha sana vile na uwezo wa kufanya ikiwa pamoja na kusoma sana vitabu anafanya vile kutafuta kuing'arisha ndoto yake itimie hivyo wamuache aje akamilishe ndoto yake" 

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Familia yatoa neno kupotea Abdul Nondo
Familia yatoa neno kupotea Abdul Nondo
https://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2018/03/07/Nondo%20Familia.jpg?itok=gNdbJRoe×tamp=1520438862
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2018/03/familia-yatoa-neno-kupotea-abdul-nondo.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2018/03/familia-yatoa-neno-kupotea-abdul-nondo.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy