Kituo cha Redio Times cha jijini Dar es Salaam kimetakiwa kuwasilisha kipindi cha mahojiano waliyofanya na mwanamuziki Diamond Platinum...
Kituo cha Redio Times cha jijini Dar es Salaam kimetakiwa
kuwasilisha kipindi cha mahojiano waliyofanya na mwanamuziki Diamond
Platinumz kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa ajili ya
uchunguzi zaidi.
Mkurugenzi wa Times FM, Amani Misana amesema kuwa amepokea
barua ya kuwataka wawasilishe kipindi hicho kilichorushwa Machi, 19,
2018 na kwamba leo wametekeleza agizo hilo.
“Tumepokea barua na tumefanya yale tuliyoagizwa ikiwamo kuwasilisha kipindi chote,” amesema kwa ufupi Misana.
Kaimu Meneja Mawasiliano wa TCRA, Semu Mwakyanjala amesema
suala la kituo hicho kupewa barua ni la kiutawala zaidi na mamlaka hiyo
haipo kwenye kitengo chake isipokuwa kama tayari barua imefika, wakati
wa kutolewa uamuzi vyombo vya habari vitaalikwa.



