Mkurugenzi wa mawasiliano na mmoja wa mashauri wa karibu wa Rais Trump wa muda mrefu ameachia ngazi yake,mamlaka imesema. Mwanamke huyo...

Mkurugenzi wa mawasiliano na mmoja wa mashauri wa karibu wa Rais Trump wa muda mrefu ameachia ngazi yake,mamlaka imesema.
Mwanamke huyo wa miaka 29 aliyekuwa mwana mitindo na mfanyakazi wa kampuni ya Trump, amekuwa karibu naye kwa miaka mingi.
Anaripotiwa kuwaambia wafanyakzai wenzake kuwa amehisi
ametimiza wajibu wake katika ikulu ya White House,Yeye ni mtu wa nne
aliyeshika nyadhifa wa mkurugenzi wa mawasiliano,Msemaji wa White House
Sarah Sanders amesema haijulikani ni lini haswa Bi Hicks ataondoka.
Amekanusha kuwa hatua hio inahusiana na ushahidi amabyo Bi
Hicks aliutoa mbele ya kamati Congress wakati aliporipotiwa kukiri
kusema uongo wa wazi kwa niaba ya Bw Trump.
Wakati wa kampeni za uchaguzi, Bi Hick alifanya kazi kama
khatibu wa mawasiliano. Alichukua nafasi wa kuungoza idara ya
mawasiliano ya White House Agosti iliopita, baada ya ufutaji kazi wa
ghafla wa Bw Anthony Scaramucci, Kabla yake , Sean Spicer na Mike Dubke
walishika nyadhifa hio.



