http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Uchaguzi Kinondoni: Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDSM apoteza maisha!

Wakat CHADEMA wanaelekea kweny ofisi ya mkurugenz kudai barua za viapo..polisi walivuruga na kuanza kupiga mabomu zikiambatana na risasi ...

FB_IMG_1518810255853.jpg
Wakat CHADEMA wanaelekea kweny ofisi ya mkurugenz kudai barua za viapo..polisi walivuruga na kuanza kupiga mabomu zikiambatana na risasi za moto..kwa wapenzi na wanachama wa CDM eneo la mkwajuni..kuna polisi alifyatua risas ambayo ilimlenga mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDSM Aqulina Akwilini..risas iliyomlenga kifuani na kupoteza maisha

Mtatiro anasema;

DAMU!

Kwa mujibu wa sheria za uchaguzi, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo analo jukumu la kutoa viapo kwa kila wakala wa kila chama cha siasa ambaye atakwenda kuwakilisha chama na mgombea wake kituoni.

Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Kinondoni (DED) ambaye pia ni kada wa CCM hadi jioni ya leo alikuwa amegoma kutoa viapo kwa mawakala wa CHADEMA na vyama vingine huku wale wa CCM wakiwa walishapewa.

Kukosa viapo kuna maana wakala hatoruhusiwa kukanyaga kituoni na CCM wangelibakia wenyewe vituoni. Baada ya kufunga kampeni jioni ya leo, Mhe. Freeman Mbowe aliambatana na mawakala kwenda kwa msimamizi wa uchaguzi (ofisini).

Wakiwa njiani wakazingirwa na magari ya Polisi huku wakishambuliwa kwa risasi za moto na mabomu. Huwezi kuamini kama mambo haya yanatokea Tanzania! Mawakala kadhaa wa CHADEMA wamepigwa risasi za moto, wengine wamejeruhiwa kwa virungu, magongo n.k.

Katika upigaji huo wa risasi za MOTO tena hovyo hovyo, INASEMEKANA KUWA Polisi wamemuua mwanafunzi wa Mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM),Aqulina Akwilini Baftaha, ambaye amepigwa risasi akiwa kwenye daladala. Mwanafunzi huyu alikuwa safari yake na wala hakuwa kwenye mkutano wa Chadema. Risasi za Polisi wetu zimemfikia huko huko, na INAELEZWA KUWA hivi sasa ni marehemu.

Nimeumia sana! Nimejeruhiwa moyoni! Roho inaniuma mno. Kwa nini? Kwa nini tunapiga watu wasio na hatia risasi za moto? Nani ametoa amri hiyo? Ni kwa nini tunashambulia watu waliokuwa wanakwenda kudai viapo vyao kwa sababu saa 11 alfajiri wanapaswa kuwa vituoni?

Kwamba baada ya DED wa Kinondoni kuwanyima viapo, mlitaka wafanyeje? Kwa nini tunaifukuza amani? Kwa nini tunaua raia wasio na hatia? Kwa nini tunavamia na kuwapiga watu hata wasio na jiwe mkononi? Kwa nini tunatumia risasi za moto kuwapiga watu wetu?

Nchi yangu inaniuma sana. Mama Tanzania anateketea!

Huyu Mkurugenzi wa Kinondoni, ametoa viapo hivyo usiku huu, baada ya watu kupigwa risasi, kina John Heche (Mbunge wa Tarime) kukamatwa, mawakala wa CHADEMA kukamatwa na mwanafunzi aliyekuwa na safati zake kuuawa.

Huyu Mkurugenzi wa Kinondoni alitumwa na nani kutoa viapo baada ya watu kufa? Nadhani sasa CCM wamo shereheni, sherehe za damu! Hawawezi kutafuta madaraka bila kumwaga damu, bila kunywa damu! Madaraka ya damu, wanaoga damu, wanafungua kinywa kwa damu, wana-lunch damu na ku-dinner damu.

Damu!

#Mtatiro

CREADITY..JAMIIFORAM
Huyu ndio mwanafunzi aliepigwa risasi na CCM na kufariki ili Mtulia aweze kuwa mbunge wa Kinondoni........Nasema hivyo sababu Kumbukeni hili tukio limetokea sababu wananchi wa kinondoni wakiongozwa na mwenyekiti wa Chadema Mbowe waliandamana hadi ofisi za Mkurugenzi kudai barua za mawakala. Kumbukeni kuwa mawakala wa Chadema wameomba hizo fomu zaidi ya wiki mbili sasa na hawapewi na video nilikuwa naposti, solution ya mwisho iliyokuwa imebaki ndo hiyo ya viongozi wa chadema kuandamana na wananKinondoni mpaka kwa mkurugenzi. Kuliko kutoa barua za mawala CCM wakaona bora kuwamwagia risasi wananchi ili tu Mtulia ashinde ubunge. . . Na nnasema CCM sababu jeshi la polisi lisingefanya unyama huu kama sio amri ya viongozi wa CCM.... . . Tanzania ndio tumefikia hapa, barua za mawakala wa upinzani haziwezi kutolewa mpaka watanzania wapoteze maisha na wengine wajuruhiwe vibaya na wengine wawekwe ndani.... These are sad times for Tanzania. Ambao bado mnaendelea kusapoti hiko chama na mwenyekiti wake mna roho ngumu sana lazma mmoja wa wazazi wenu atakuwa na asili ya Rwanda au Congo. Hamuwezi kuwa watanzania full alafu mkasapoti chama kinachofanya ukatili kama huu kwa watanzania wenzenu.... . . Simjui huyu mtoto ila nimeliaaaaaa kama nna undugu nae..R.I.P Aquilina
A post shared by Mange Kimambi (@mangekimambi_) on

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Uchaguzi Kinondoni: Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDSM apoteza maisha!
Uchaguzi Kinondoni: Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDSM apoteza maisha!
https://www.jamiiforums.com/attachments/fb_img_1518810255853-jpg.696688/
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2018/02/uchaguzi-kinondoni-mwanafunzi-wa-mwaka.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2018/02/uchaguzi-kinondoni-mwanafunzi-wa-mwaka.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy