Mwanasiasa mkongwe na kada wa Chama cha kidemokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tambwe Hizza amefariki dunia asubuhi ya kuamkia leo (Alhami...

Mwanasiasa mkongwe na kada wa Chama cha kidemokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) Tambwe Hizza amefariki dunia asubuhi ya kuamkia leo
(Alhamis ) akiwa nyumbani kwake.
Taarifa hiyo imethibitishwa na mgombea Ubunge wa Jimbo la
Kinondoni ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Salum Mwalimu
alipowasili katika kipindi cha 'East Africa Breakfast' kinachorushwa
kutoka East Afrika Radio.
"Ni kweli Tambwe Hizza amefariki nami nimetumiwa ujumbe
mfupi mara nilipofika hapa East Afrika Radio kama kiongozi wa chama,
hivyo naomba tupewe muda kidogo ili tuweze kufahamu zaidi chanzo cha
kifo chake maana imekuwa ghafla sana kutokana mpaka jana usiku saa 5
nilikuwa nae", amesema Mwalimu.
Kwa upande mwingine, Salum Mwalimu amesema mpaka jana
marehemu Tambwe Hizza alikuwa nae katika kuomba ridhaa kwa wananchi wa
jimbo la Kinondoni ili aweze kuwa Mbunge wa Jimbo hilo katika siku za
usoni.



