Hali ya Maendele ya Afya ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ,Charles Mkumbo ambaye amelazwa katika hospitali ya mkoa Mount Meru baada...
Hali ya Maendele ya Afya ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Arusha ,Charles Mkumbo ambaye amelazwa katika hospitali ya mkoa Mount
Meru baada ya kupata ajali jana akitokea Mkoani Singida inaendelea
vizuri.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake
mganga mkuu wa Hospitali hiyo ,Jackline Urio amesema kuwa wamelazimika
kumpumzisha katika chumba cha wagonjwa mahututi( ICU) ili apate muda
mzuri wa kupumzika na hali yake ni nzuri.
"Hospitali yetu haina vyumba binafsi vya wagonjwa ndio
maana tumeamua kumpumzisha chumba cha ICU na sio kwamba yupo mahututi
hali yake ni nzuri"Amesema
Aidha amesema kwamba Mkumbo alifikishwa katika hospitali
hiyo jana majira ya jioni na kufanyiwa upasuaji baada ya kuumia sehemu
ya Kichwa ,na kidole cha mkono wa kushoto ambacho kimevunjika.
Hata hivyo mganga mkuu amesema kuwa pamoja na afya ya
majeruhi kuendelea vizuri anapaswa kutumia muda mwingi kupumzika
kutokana na majeraha kichwani yaliyotokana na kukatwa na vyoo vya gari.
Watu mbalimbali mashuhuri wamekuwa wakimiminika katika
hospitali hiyo kwà lengo la kumjulia hali ingawa uongozi wa hospitali
hiyo umezuia kumwona
Naye kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ,Yusufu Ilembo
,amesema kuwa mkumbo alipata ajali jana majira ya saa 8 mchana katika
eneo la Mdorii ,wilayani Babati mara baada ya gari alilokuwa akitumia
lenye namba PT 2040 kupasuka tairi la nyuma na kupinduka.
Mkumbo alikuwa akitumia gari la polisi aina ya Landcruser
V8,lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyetambuliwa kwa jina la staff
sajenti Silvanus ambaye naye alipata majeraha ya mguu huku mlinzi wa
kamanda huyo akitoka mzima wa Afya.
Aliongeza kuwa huenda akaruhusiwa siku za usoni kuanzia kesho kutokana na halinyake kutengamaa.
Mwisho



