Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob amesema kuwa viongozi wengi wa serikali wanapendelea upande mmoja wa msiba wa Akwilina kwani hata wao c...

Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob amesema kuwa viongozi wengi
wa serikali wanapendelea upande mmoja wa msiba wa Akwilina kwani hata
wao chadema wamekuwa wakipata misiba lakini serikali haitoi pole wala
kuwafariji wafiwa.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam jana wakati wa kuaga
mwili wa kada wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Daniel
John.
Alisema kuwa kitendo cha viongozi wa serikali kutoenda
kutoa pole katika familia ya Daniel John na kuegemea upande mmoja wa
msiba wa familia ya Akwilina ni fedhea kubwa.
“Kwakweli hii ni fedhea kubwa sana kwa viongozi wa serikali
kuegemea upande mmoja kwenye msiba wa Akwilina, hii si haki kwani
wangekuja hata huku kutoa angalau salamu za pole na kuwafariji wafiwa,
kwani kifo cha Daniel kinasikitisha sana,”alisema Jacob
MSIKILIZE HAPA
MSIKILIZE HAPA



