Bweni la wasichana wa shule ya sekondari Kipoke mkoani Mbeya limeteketea kwa moto na kusababisha uharibifu mkubwa huku wanafunzi wa...

Bweni la wasichana wa shule ya sekondari Kipoke mkoani Mbeya limeteketea kwa moto na kusababisha uharibifu mkubwa huku wanafunzi wawili wakijeruhiwa.
Hayo yamethibitishwa na Mkurugenzi wa shule hiyo Gervas
Mwanyila wakati alipokuwa anazungumza na mwandishi wa habari wa EATV na
kusema ni kweli tukio hilo limetokea katika shule yao japokuwa mpaka
sasa hawajafahamu chanzo chake.
"Ni bweni la wasichana kidato cha pili limeungua moto
ambapo mpaka sasa hatujajua chanzo chake kama ni umeme au ni wanafunzi
wenyewe tumeshindwa kufahamu. Tumefanya jitihada za kunusuru vitu vya
wanafunzi na wao wenyewe lakini tumefanikiwa kwa kiasi kidogo kutokana
na baadhi ya vitu ikiwemo magodoro na vitanda 68 kuteketea na moto",
amesema Mwanyila.
Pamoja na hayo, Mwanyila ameendelea kwa kusema "ni
vijana watano pekee waliojeruhiwa kidogo na moto huo baada ya wao
kusaidia kukata bati ili moto usiweze kuenea katika maeneo mengine ya
bweni".
Kwa upande mwingine, Mwanyila amesema bado hawajaweza
kujuwa tathimini kamili ya mali za shule zilizoweza kuteketea na moto
kutokana bado hawatulia tokea ajali hiyo ya moto ilipoanza.



