Watu wanne wamefariki dunia na moja kujeruhiwa vibaya baada ya kuangukiwa na kifusi cha mchanga aina ya Moramu katika machimbo ya mchan...

Watu
wanne wamefariki dunia na moja kujeruhiwa vibaya baada ya kuangukiwa na
kifusi cha mchanga aina ya Moramu katika machimbo ya mchanga yaliyopo
kata ya Murieti jijini Arusha wakati wakipakia mchanga katika machimbo
hayo.
Tukio hilo limetokea mapema Jana,jan,30 majira ya saa tano asubuhi katika eneo la mlima wa ccm Kata ya murieti
Marehemu wametambulika
kwa majina ya Yusufu Mohamed Kamwende(35),Athumani Husein Luvanda,na
Richard Kishimbo(57) na mmoja bado hajatambulika
Katika
tukio hilo dereva wa gari lililokuwa likipakia Moramu aliye tambulika
kwa jina moja la Hamisi alipata majeraha sehemu za kichani na kuvunjiaka
mkoano ambapo amelazwa katika hospitali ya mkoa Mount Meru kwa matibabu
zaidi.
Mashuhuda
wa tukio hilo akiwemo diwani wa kata ya Muriet,Francis Mbise ameeleza
kuwa marehemu walifariki dunia wakati wakipakia Moramu katika gari hilo
ndipo ghafla ngema ilipokatika na kuwafunika ,
Aidha aliongeza kuwa gari aina ya Isuzu mali ya majeruhi iliyokuwa ikipakia Moramu hiyo iliharibika vibaya .
Kamanda
wa polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amethibisha tukio hilo na kusema
kwamba si mara ya kwanza kutukea tukio kama hilo ambapo amewataka
wataalamu kutoka jiji la Arusha kutembelea katika machimbo hayo na kutoa
tathimini iwapo machimbo hayo yanafaa kuendelea kuchimbwa ama
yasitishwe ili kuepuka maafa zaidi kama hayo yanayoweza kujitokeza.
Aidha
amewataka wajimbaji wa Moramu kuchukua tahadhali pale wanapoona kuna
tishio la ngema kumeguka ili kuepuka na hatari iliyopo mbele yao




