http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Jenerali wa Jeshi ampa Rais Kabila siku 45 aachie Urais, asambaza video

Haijapita hata miezi mitatu toka tushuhudie Jeshi likiingilia kati na kumuondoa madarakani Rais aliekaa muda mrefu madarakani, Robert Mu...

Haijapita hata miezi mitatu toka tushuhudie Jeshi likiingilia kati na kumuondoa madarakani Rais aliekaa muda mrefu madarakani, Robert Mugabe wa Zimbabwe….. leo tena tunasikia huko Congo DRC Mwanajeshi mmoja ampa Rais Kabila siku 45 awe ameachia madaraka.
Tunafahamu kwamba Rais Kabila alimaliza muhula wake wa pili na wa mwisho kikatiba kuwa Rais mwezi December 2016 lakini hajaachia madaraka, mengi yamesemwa na Serikali ikiwemo “hatuna pesa za kutosha kufanya Uchaguzi Mkuu”
January 19 2018 Mwandishi wa habari Byobe Malenga alieko Congo DRC ameiambia millardayo.com kwamba Jenerali mmoja wa Jeshi aitwae John Tshibangu ameasi na kutangaza vita na Rais Kabila, amempa siku 45 aachie madaraka.
John Tshibangu
Asubuhi ya Ijumaa January 19 2018 Wanajeshi walionekana kuizingira kwa wingi IKULU ya Kinshasa huku video iliyorekodiwa na Jenerali Tshibangu ikiendelea kusambaa ambapo ndani yake ameonekana kazingirwa na Wanajeshi wenye silaha.
Kwenye video hiyo Tshibangu amenukuliwa akisema “Nafahamu siri ya Rais Kabila, sasa ni muda wa kuondoa Serikali ya Mabeberu na Udikteta, na ni lazima Rais Kabila aombe msamaha kwa Wakongo kuanzia Makanisani, Shuleni na hata Raia wa kawaida kwa kosa la kushindwa kuiongoza Nchi”
“Mimi kama Mwananchi mwenye msimamo na huruma kwa mateso yenu, niliamua kujitokeza ili kumfukuza Joseph Kabila kwa nguvu za vita na kijeshi, nawahakikishia kwamba tutamuwinda na atakimbia. ” – John Tshibangu.
Rais Kabila – picha ya REUTERS/Kenny Katombe
Tshibangu amelitaja kundi lake la Waasi kwamba linaitwa Forces Nouvel du Congo ikimaanisha NGUVU MPYA KWA AJILI YA CONGO ambapo Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa kumekuwa na majaribio ya mapinduzi katika Serekali ya Congo ambapo IKULU ya Taifa imezungukwa na Wanajeshi wengi wanaoonekana kama Wageni, yaani sio Wanajeshi wa congo.
Raisi Kabila amekabiliwa na upinzani mkali kutokana na nia yake ya kutaka kugombea Urais kwa muhula wa tatu baada ya muhula wake wapili kumalizika mwezi December 2016.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Jenerali wa Jeshi ampa Rais Kabila siku 45 aachie Urais, asambaza video
Jenerali wa Jeshi ampa Rais Kabila siku 45 aachie Urais, asambaza video
http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2018/01/19232426/Screen-Shot-2018-01-19-at-10.12.34-PM-660x400.png
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2018/01/jenerali-wa-jeshi-ampa-rais-kabila-siku.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2018/01/jenerali-wa-jeshi-ampa-rais-kabila-siku.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy