Msemaji wa upinzani wa Wizara ya Katiba na Sheria, Ally Salehe amesusa kusoma maoni ya upinzani ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mba...
Msemaji wa upinzani wa Wizara ya Katiba na Sheria, Ally
Salehe amesusa kusoma maoni ya upinzani ya Muswada wa Marekebisho ya
Sheria Mbalimbali baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kukataa
kusomwa kwa baadhi ya maneno yaliyomo katika maoni hayo.
Salehe alikuwa akisoma maoni hayo leo Januari 30 mwaka 2018
kwa niaba ya msemaji wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu aliyeko
nchini Ubelgiji kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi Novemba 7
mwaka jana.
Maneno yaliyozuiwa na Chenge kusomwa na upinzani ni kuhusu matukio ya uhalifu nchini, likiwemo la kushambuliwa kwa Lissu.
Salehe alianza kusoma maneno hayo lakini alipofika aya ya
nne alikatizwa na Chenge akimtaka asubiri, baadaye kumueleza kuwa lugha
iliyotumika katika ukurasa kwa kwanza na pili wa hotuba hiyo si ya
kibunge.
Baada ya kauli hiyo, Salehe amesema upinzani unaiamini na
unaisimamia hotuba hiyo kwa kuwa wabunge wote wanayo nakala yake,
akaomba kuiwasilisha na kurejea kuketi.



