POLISI wilayani Kayunda nchini Uganda inawatafuta watu waliojaribu kulifukua kaburi la marehemu Ivan Ssemwanga lililoko katika kijiji ch...
POLISI wilayani Kayunda nchini Uganda
inawatafuta watu waliojaribu kulifukua kaburi la marehemu Ivan Ssemwanga
lililoko katika kijiji cha Nakaliro usiku wa Jumanne iliyopita ili
kuutoa mwili wake. Ssemwanga alizikwa kijijini kwao huko Mei mwaka huu
katika mazishi yaliyokuwa na shamrashamra kibao.

Shimo kubwa kwenye kburi la Ivan.
Habari zilizopatikana kutoka kwa mmoja
wa ndugu zake zimesema waliofanya hivyo walikuwa wamelenga kulichukua
fuvu lake. Kaburi lake lilikuwa likilindwa na polisi kuzuia watu
wasilifukue na kuchukua fedha ambazo zilitupwa ndani ya kaburi hilo na
marafiki zake waliokuwa wanajiita “kundi la matajiri”.

Kaburi la Ivan lilivyofukuliwa.
“Nilikuwa nikipita karibu na kaburi
majira ya saa saba mchana na niliona shimo kwenye kaburi la Ssemwanga.
Nilisogea karibu kuona nini kilikuwa kimetokea,” alisema Ali
Wamala, mmoja wa ndugu wanaoishi nyumbani hapo. Hata hivyo, alidai
kwamba huenda waganga wa kienyeji walikuwa nyuma ya njama za kuufukua
mwili wa Ssemwanga.

Kaburi lilivyofukuliwa.
Polisi walililinda kaburi hilo kwa
zaidi ya mwezi mzima. Naye Naibu Mkuu wa wilaya hiyo, Yahaya Were,
amesema upelelezi umeanza na watuhumiwa watakaokamatwa watafikishwa
mahakamani. “Hili ni suala la usalama na polisi wameanza uchunguzi dhidi
ya watu wanaotaka kuharibu amani ya wafu,” aliongeza Were.

Kaburi la Ivan likiwa na limetapakaa noti.
Tangu kuzikwa kwa Ssemwanga, ndugu zake
walikodi walinzi kulinda kaburi hilo lakini habari za kuaminika
zimesema walishindwa kuwalipa mishahara yao kwa mujibu wa makubaliano
yaliyofikiwa. Inasemekana walinzi hao mwezi wa kwanza walilipwa Sh.
600,000 mbali na kwamba walikuwa wamekubaliana kuwalipa Sh. milioni
moja.