ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera , amefariki dunia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa ak...
ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, amefariki dunia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiowa matibabu.
Kwa mujibu wa Waziri wa Zamani wa Maliasili na Utalii, Hamis Kagasheki ameandika kwenye mtandao wake wa twitter;
“Nimepokea kwa mstuko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Ndg Joel Bendera.
Alilitumikia Taifa letu kwa jitihada kubwa. Kwa kutaja machache,
aliwahi kuwa Mbunge, Naibu Waziri, Mkuu wa Mikoa kadha nk. Pole zangu
kwa family, ndugu, rafiki,wa marehemu. Rest in peace Joel,” ameandika
Kagasheki




