Moja ya habari kubwa kutokea Bungeni Dodoma leo November 17, 2017 ni pamoja na kauli ya Serikali kuhusu kubadilisha utaratibu ambao umeku...
Moja ya habari kubwa kutokea Bungeni Dodoma leo November 17, 2017 ni pamoja na kauli ya Serikali kuhusu kubadilisha utaratibu ambao umekua ukitumika na wenye nyumba kwamba Mpangaji yeyote ni lazima alipie kodi ya pango kwa miezi 6 hadi mwaka. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula alitolea ufafanuzi baada ya kuulizwa swali na Mbunge wa viti maalum CCM Halima Bulembo aliyehoji Serikali ni lini itabadilisha sheria hiyo.
Serikali kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema kuwa iko kwenye mchakato wa kuanzisha mamlaka itakayo simamia masuala ya kodi ya nyumba itakayo fanya ukomo wa kodi kulipwa kwa mwezi mmoja na si miezi sita wala kumi na mbili.
Hayo yamezungumzwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Angelina Mabula wakati akijibu swali la Mbunge Halima Bulembo aliyehoji
Je, ni lini sasa serikali itafuta utaratibu wakulipa kodi kwa miezi 6 au mwaka na sisi kama bunge tutunge sheria itakayo walazimisha wamiliki wote kupokea kodi ya kila mwezi badala ya mwaka au miezi sita kama ilivyo sasa?
“Naomba nimtaarifu Mhe. Mbunge pamoja na wabunge wizara tayari imekwisha liona hilo, na tayari tuko kwenye mchakato wa kuanzisha mamlaka itakayo simamia masuala yote ya nyumba na katika sheria, na hiyo sheria italetwa hapa bungeni. Tumeangalia suala la ukomo wa kutoa kodi za nyumba hiyo ya miezi sita na mwaka mmoja haita kuwepo,amesema Mabula.
“Tumeona inaumiza watu wengi kwahiyo kodi itakuwa inalipwa kwa mwezi mmoja mmoja na wakati huo huo utatakiwa kuweka kama amana ya miezi mitatu kwaajili ya shughuli zingine ambazo zinaweza kuwa, kwahiyo suala hilo limelisikia na tunalifanyia kazi ,” amesema Mabula.



