TAKUKURU wamesema wameshangazwa na Wabunge Nassari na Lema kuongea na waandishi baada ya kuwapa ushahidi, na walicholeta Lema na Nassari ...

TAKUKURU wamesema wameshangazwa na Wabunge Nassari na Lema kuongea na waandishi baada ya kuwapa ushahidi, na walicholeta Lema na Nassari sio ushahidi ni taarifa na wanaifanyia kazi
Katika ushahidi kuna mambo mengi na wanaangalia matakwa ya kisheria, ushahidi una relevance na possibility
Sheria inataka mtoa taarifa alindwe lakini Nassari na wenzake walifanya watu kuwafahamu kwa kuongea na waandishi wa habari
Pia ametoa Onyo kwa Nassari wasiwe wanaishinikiza chombo hicho na kukiweka kwenye malumbano ya kisiasa
Amemshangaa Nassari kuuliza kwa nini hawajaupeleka ushahidi huo mahakamani mpaka sasa na kusema wao wanaongozwa na sheria ya mwenendo wa mashtaka na wakishamaliza uchunguzi watatathimini matokeo waliyoyapata na wakijiridhisha walichopewa kinakidhi vigezo vilivyowekwa na sheria watafikisha katika hatua nyingine ya mwenendo wa mashtaka ya jinai na watapeleka mashataka kwa mwendesha mashataka mkuu wa serikali na ataandaa mashataka dhidi ya washtakiwa kama wapo
Uchunguzi unaweza kugundua walichopeleka ni kosa ama sio kosa, inawezekana kuna matukio yanafanyika na watu wanadhani ni makosa kumbe ni 'moral wrongs' tu amabayo yanahitaji utaratibu mwingine wa kuwashukulikia
Amemshauri Nassari kukoma mara moja kugeuza mchakato huo wa kisheria kuwa malumbano ya kisiasa



