Spika wa bunge la wawakilishi la Ethiopia Abadula Gemeda amewasilisha barua ya kujiuzulu jana Jumapili. Kiongozi huyo ni miongoni mwa maa...
Spika wa bunge la wawakilishi la Ethiopia Abadula Gemeda amewasilisha barua ya kujiuzulu jana Jumapili.
Kiongozi huyo ni miongoni mwa maafisa wa juu kufanya hivyo tangu utawala wa muungano wa EPRDF ulipoingia madarakani mwaka 1991.
Gemeda hajabainisha sababu za kujiuzulu lakini amesema atafanya hivyo pindi bunge litakaporidhia uamuzi wake huo.
Wachambuzi wa masuala ya nchi hiyo ya pembe ya Afrika wanasema Gemeda ambaye anatoka katika kabila la Oromo huenda ameamua kuachia madaraka kwa kutokukubaliana na namna serikali ilivyoyashughulikia machafuko yaliyoukumba mkoa wa Oromiya mwaka 2015 na 2016.
Machafuko hayo yaliilazimisha serikali kutangaza utawala wa hali ya hatari kwa miezi tisa, amri ambayo iliondolewa mwezi Agosti.



