Mbunge Godbless Lema amefunguka na kusema maneno aliyosema IGP Sirro jana kuhusu dereva wa Lissu ni dhihaka kubwa kwa...
Mbunge Godbless Lema amefunguka na kusema maneno aliyosema IGP Sirro
jana kuhusu dereva wa Lissu ni dhihaka kubwa kwa ndugu wa Lissu,
wanachama wa CHADEMA na hata viongozi wa chama hicho na kusema
hakustahili kusema maneno yale kama IGP.
Lema amesema hayo baada ya IGP Sirro kusikika katika baadhi ya vyombo vya habari akiwa Mtwara akisema kuwa dereva wa Tundu Lissu ndiyo anachelesha uchunguzi wa sakati hilo hivyo aliomba arudi ili kulisaidia jeshi la polisi kutoa taarifa ili kufanikisha upelelezi wa sakata la kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.
Lema amesema hayo baada ya IGP Sirro kusikika katika baadhi ya vyombo vya habari akiwa Mtwara akisema kuwa dereva wa Tundu Lissu ndiyo anachelesha uchunguzi wa sakati hilo hivyo aliomba arudi ili kulisaidia jeshi la polisi kutoa taarifa ili kufanikisha upelelezi wa sakata la kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.
"Kamanda Sirro amesikika
akiwa Mtwara akisema jeshi la polisi linamuhitaji dereva wa Tundu Lissu
kwa ajili ya kukamilisha mahojiano ya upelelezi na kwamba tunasema au
CHADEMA inasema anaumwa wakati dereva akionekana akipiga picha anang'ara
kabisa, hii ni lugha ya mzaa na lugha ya kadhia hasa kwa familia na
sisi wanachama wenzake na Tundu Lissu na hasa kwa dereva mwenyewe ambaye
alishuhudia na kusikia milio ya risasi zaidi ya 30 na leo si tu kwamba
anatatizo la kisaikolojia kwake binafsi lakini amuona boss wake, kaka
yake na mzee wake wa siku nyingi akiwa kitandani akisubiri kudra za
Mwenyezi Mungu kuweza kuishi hivyo hii ni kauli ya mdhaa ni kauli ambayo
haikupaswa kutolewa na IGP" alisema Lema
Mbali na hilo Lema amelitaka jeshi la polisi kukamilisha kwanza
upelelezi wa matukio ya kupotea kwa Msaidizi wa Mbowe, Ben Sanane kifo
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo ambao wao hawakuwa
hata na madereva lakini mpaka sasa jeshi la polisi limeshindwa kutoa
ripoti juu ya matukio hayo.
"Leo wanaposema dereva wa
Lissu anachelewesha upelelezi kukamilika siyo kweli kwa sababu Ben
Sanane hakuwa na dereva na mpaka leo hatujawahi kuona mchakato wa suala
lake kukamilika, Mawazo pia hakuwa na dereva lakini mpaka leo
tunaushuhuda kwamba waliopo jela walishawahi kugoma barabarani na kusema
wao hawakuwa wahusika wa tukio lile, wapo watu wengi wa CHADEMA
wameuwawa lakini hawakuwa na madereva kama wameshindwa kukamilisha
kwanza upelelezi huo ni mtake kwanza Sirro akamilishe kwa haraka suala
la Ben Sanane ambalo kimsingi wamekataa kufanya utafiti wake, tunajua
serikali haiwezi kufanya uchunguzi wa tukio la Lissu kwa sababu wanajua
nini kimefanyika" alisema Lema



