Baada ya Rais Magufuli kuhutubia Arusha katika shughuli za kuwatunukia Kamisheni Maafisa ya Jeshi la Wananchi JWTZ na ...
Baada ya Rais Magufuli kuhutubia Arusha katika shughuli za kuwatunukia
Kamisheni Maafisa ya Jeshi la Wananchi JWTZ na kisha kuwapa nafasi
Madiwani kumi waliohama Chadema kwa madai ya kumuunga Rais mkono Wabunge
wa Arusha wametaka kukutana na Rais
ili wamuoneyeshe rushwa ilivyotumika na watumishi wake.
ili wamuoneyeshe rushwa ilivyotumika na watumishi wake.
Kupitia ujumbe wa Video uliowekwa na
viongozi hao mtandaoni, Godbless Lema wa Arusha Mjini pamoja na Joshua
Nassari wa Arumeru Mashariki wamemtaka Rais Magufuli kuwapatia nafasi za
kuweza kumthibitishia jinsi viongozi wake walivyoweza kutumia rushwa na
kuwashawishi madiwani hao wa Chadema kuachia ngazi na kumhakikishia
kuwa ushahidi wote wanao hivyo wao wapo tayari kumuonyesha hata mbele ya
vyombo vya usalama.
Mh. Lema amesema kuwa wao kama Chadema
hawana shida kwa viongozi hao kuondoka ndani ya chama chao na hata kama
wataondoka wote, lakini wanachosikitika ni jinsi viongozi hao
walivyofanya vitendo vya aibu na vya kumdhalilisha Mh. Rais kwa kutumia
rushwa.
"Tuna taarifa tulizipata
kwamba leo madiwani wawili wa Arusha mjini wangeondoka na kujiunga na
CCM lakini kwetu siyo shida, Mh. Rais anapaswa kufahamu kwamba hakuna
chochote kitakachofanyika kwenye ofisi za Mkuu wa mkoa, Mkuu wa Wilaya
au Mkurugenzi ndani ya Arusha na sisi tusikipate. Sasa Mh. Rais. Mimi
nataka umuite Nasarri, RPC, IGP na hata Takukuru tukupatie ushahidi.
Mimim sitaweza kuja maana najua sipendwi sana.
Ameongeza kwamba "Tulikuwa
tunasubiri tukio la leo, wewe ni Rais mcha Mungu na Kiongozi unayepinga
Rushwa, hawa watu wanaosema wamejiunga na Chama chao utajua wamejiunga
kwa sababu ya kukuunga mkono au wameunga rushwa na fedha mkono. Hawa
watu walioandaa hafla Mh. Rais wamekutia aibu sana na tutoe angalizo
kwamba ushahidi huu haupo nyumbani kwetu msije kutufata upo hewani na
mkituletea shida tutawaambia vijana wabonyeze Button ili usambae au pia
usikutana na Nassari tutauachia.
Kwa Upande wa Mbunge Joshua Nassari
amesema kesho watafanya mkutano na wanahabari na kuelezea rushwa
ilivyotumika na viongozi kumdanganya Rais wa nchi na kusisitiza ushahidi
wao hauna mashaka.



